Programu ya kuchati na kupiga simu ya Skype imekuja na uwezo mpya kuanzia sasa utakaopatikana kwa watumiaji wote duniani kote, uwezo wa kuchati au kuongea katika lugha tofauti na mtu mwingine na meseji zenu kuweza kutafsiriwa muda huo huo na hivyo kuelewana.
Kampuni ya Skype inayomilikiwa na kampuni kubwa ya Microsoft ilishatangaza kuwa inatengeneza teknolojia hiyo tokea mwaka jana, na sasa watu wote wanaotumia programu endeshaji wa Windows wataanza kutumia teknolojia hiyo.
Inafanyaje Kazi?
- Fikiria kuna mtu mmoja anajua kiingereza tuu wakati mtu mwingine anazungumza kihispania tuu
- Mmoja akiandika meseji/ujumbe na kumtumia mwingine ujumbe huo utapokelewa ukiwa katika lugha atakayoichagua yeye ili kumuwezesha msomaji kuweza kuuelewa katika lugha yake.
- Naye akijibu katika lugha yake msomaji wa upande wa pili ataupokea katika lugha yake.
- Kwa kupiga simu utafsiri huo utafanyika na kuweza kusomeka kwa maandishi
- Katika kuchati mpokeaji atapokea meseji katika lugha zote mbili, ya mtumaji ya yeye msomaji.
Kwa sasa uwezo huo wa utafsiri lugha kwa watu wanaopigiana simu unafanya kazi kwa lugha ya kiingereza, kihispania, kiitaliano na kichina (mandarini), wamesema wanategemea kuweza kuongeza lugha zingine taratibu.
Ila kwa wanaochati kwa kutumia kuandikiana ujumbe teknolojia hii inafanya kazi kwa zaidi ya lugha 50, kwa sasa kiswahili si moja ya lugha hizo, ila tutegemee itakuja hapo mbeleni.
Arabic | English | Hungarian | Maltese | Slovak | Yucatec Maya |
Bosnian (Latin) | Estonian | Indonesian | Norwegian | Slovenian | |
Bulgarian | Finnish | Italian | Persian | Spanish | |
Catalan | French | Japanese | Polish | Swedish | |
Chinese Simplified | German | Klingon | Portuguese | Thai | |
Chinese Traditional | Greek | Klingon (plqaD) | Queretaro Otomi | Turkish | |
Croatian | Haitian Creole | Korean | Romanian | Ukrainian | |
Czech | Hebrew | Latvian | Russian | Urdu | |
Danish | Hindi | Lithuanian | Serbian (Cyrillic) | Vietnamese | |
Dutch | Hmong Daw | Malay | Serbian (Latin) | Welsh |
Kuwezesha teknolojia hii katika Skype yako itabidi ushushe na kupakua programu ya Skype Translator katika kompyuta yako yenye programu ya Skype.
Shusha Skype (Bofya) | Skype Translator (Bofya)
No Comment! Be the first one.