fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps Kompyuta Maujanja Windows

Programu za Lyrics kwenye Kompyuta, MiniLyrics na LyricsX. #Windows #Macs

Programu za Lyrics kwenye Kompyuta, MiniLyrics na LyricsX. #Windows #Macs
Spread the love

Programu za lyrics kwenye kompyuta zinaweza zikawa ni moja ya programu muhimu kwa wapenda muziki. Hizi ni programu ambazo kwa kutumia intaneti zinatafuta, kudownload na kuonesha lyrics za nyimbo unazocheza kwenye kompyuta yako. Na mara nyingi ni kwa mfumo wa karaoke.

Leo tunakuletea programu maarufu za kuonesha lyrics kwenye kompyuta zinazotumia Windows na zile za Macs.

SOMA PIA  Wadukuzi 10 hatari zaidi wa kompyuta duniani!

Kwenye Windows: MiniLyrics

programu ya lyrics kwenye kompyuta

Muonekano wa MiniLyrics inapofanya kazi kwenye kompyuta ya Windows 10

 

MiniLyrics ni programu ya miaka mingi sana na bado inafanya kazi vizuri. Ukiipakua inatambua player za muziki ulizonazo na basi kuanzia hapo ukifungua player ya muziki na programu yenyewe pia inajifungua na kuanza kuonesha lyrics.

SOMA PIA  Ifahamu App ya Metal, App Mbadala kwa Matumizi ya Facebook

Kudownload MiniLyrics – FileHippo

Kwenye Mac: LyricsX

programu ya lyrics kwenye kompyuta

Kwa chini, muonekano wa programu ya LyricsX ikiwa inafanya kazi

 

LyricsX nayo inafanya kazi kwa mfumo kama wa MiniLyrics. Kumbuka programu zote hudownload vijifaili vya lyrics, ambazo mara zote ni vidogo sana. Chini ya kb kadhaa. Utakapocheza nyimbo ile ile tena programu hizi hazidownload tena, zinasoma faili ambalo tayari lipo kwenye kompyuta yako.

SOMA PIA  Windows 10 Bure Kwa Wengi Ila Itakuwa Tsh Laki 2 Kwa Wengine

Kudownload LyricsX: AppStore

Soma maujanja zaidi – Teknokona/ Maujanja

Je ni programu za namna gani ungependa kuzifahamu zaidi pia? Tueleze kwenye comment. Kumbuka kushare na kuungana nasi kwenye mitandao ya kijamii.

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania