fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Infinix Smartphones

FAHAMU: Jinsi Ya Kuongeza RAM Mwenyewe Katika Simu Za Infinix Note 11!

FAHAMU: Jinsi Ya Kuongeza RAM Mwenyewe Katika Simu Za Infinix Note 11!
Spread the love

RAM siku hizi imekuwa feature ya muhimu kutokana na program nyingi kwenye simu za kisasa kuhitaji nguvu kubwa ya uendeshaji. Simu mpya za kama……

…….aina ya Infinix NOTE 11 Pro yenye 8GB RAM itaweza kuwa na uwezo wa kuruhusu kuongezeka RAM hadi 5GB kwa kugusa kitufe tu inatoka 8GB RAM na kuwa 13GB RAM (8GB RAM+5GB RAM = 13GB RAM).

Infinix Note 11 Pro

Infinix Note 11 Pro

Haya ni mapinduzi ya kitekinolojia ambapo sasa utaweza kutumia Applications nyingi kwa wakati mmoja bila kumaliza chaji ya simu haraka wala kustaki.

SOMA PIA  Baada ya Huawei Mate 10 kutoka sasa ni zamu ya Huawei Mate 10 Pro

Kuongezeka kwa RAM kutakusaidia kuweza kufungua Apps nyingine kwa wakati mmoja kwa kasi kutoka 802ms mpaka 307ms ambapo kasi imeongezeka kwa asilimia 61%.

RAM Iliyoongezwa Katika Simu Janja Za Infinix Note 11

RAM Iliyoongezwa Katika Simu Janja Za Infinix Note 11

Utendaji wa RAM wa NOTE 11Series unapatikana kwenye Infinix NOTE11 Pro / NOTE 11. Kwa kuwasha RAM Iliyoongezwa, simu inaweza kupakia michezo (games)  kwa kasi na kuhakikisha kuwa watumiaji wanaweza kuanza mchezo mara moja, hata ikiwa utabadili na kufungua programu nyingi.

SOMA PIA  Simu janja chini ya nusu ya asilimia moja ndio zinatumia Oreo #Ripoti

Hizi hapa hatua nne za kufuata kuongeza RAM kwenye simu za NOTE 11Series.

  • 1️⃣ Ingia Katika Setting
  • 2️⃣ Nenda Katika Eneo La Special Function
  • 3️⃣ Ingia Katika MemFusion
  • 4️⃣ Washa MemFusion Na Kisha Chagua Ni Kiasi Gani Cha RAM Unataka Kuongeza
  • 5️⃣ I’Restart Ili Iweze Fanya Kazi  

Infinix Imekuwa ikija na kuanzisha teknolojia kubwa na  mpya kwenye simu zake na bado simu zake zimekuwa zikiuzwa kwa bei rafiki.

Ongeza RAM Katika Toleo La Simu Janja Za Infinix Note 11

Ongeza RAM Katika Toleo La Simu Janja Za Infinix Note 11

RAM kuogezeka ni moja ya teknolojia ambayo Infinix wamepanga kuifanya endelevu kwa simu zote zijazo. Kwa maelezo zaidi tembelea kurasa za Infinix Tanzania kupata ufafanuzi zaidi.

SOMA PIA  Mwanzilishi mwenza wa Apple aamua kuikacha iPhone X

Timu nzima ya TeknoKona inaipongeza kampuni ya Infinix kwa kuleta mapinduzi haya katika simu janja

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii

  Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania