Kompyuta ni kifaa ambacho ni tofauti kabisa na vingine kama vile magari na baadhi ya vifaa vya nyumbani. Vifaa vingi vinaweza kukaa kwa muda mrefu sana, lakini ukiangalia kompyuta inaweza kukaa kwa miaka mine au zaidi lakini katika maisha hayo unaweza ukawa ushafanya matengenezo mengi tuu.
Lazima itakubidi kushusha matoleo mapya kama vile ya program endeshaji (OS) ili kuhakikisha tuu kwamba kompyuta yako inakua na kasi katika kufanya mambo mbalimbali na kuwa na ulinzi zaidi. Sawa ni jambo jema lakini kumbuka kuwa haya yote yanahitaji au yanachukua sehemu ya mfuko wako
Lakini badala ya kufanya hayo yote, kunaweza kukawa na njia mbadala ambayo ukiifanya unaweza kutumia kompyuta yako ya zamani ikawa kama mpya tuu.
Hiyo njia unayoisubiria kuijua kwa hamu ni kubadilisha programu endeshaji ya kompyuta hii kutoka katika Windows kwenda katika program endeshaji yoyote ambayo sio Windows.
Programu endeshaji ambazo sio za Windows ni nzuri na zina uwezo mkubwa hata katika kompyuta za zamani. Vile vile zina uwezo mkubwa wa kugeuza kompyuta zamani kutoka kwenye kutotegemewa mpaka kwenye kutegemewa na ufanisi wa kompyuta hiyo kuongezeka.
TeknoKona tunashauri uchague progaramu endeshaji kutoka Linux, sababu ni kwamba hii ni ya bure, ina usalama wa hali ya juu na ina matoleo ambayo yanafanya kazi vizuri katika kompyuta za zamani kuliko Windows.
Kama utaona programu endeshaji ya Linux labda ni ngumu kwako au inakupa shida katika kutumia kumbuka zipo programu endeshaji nyingi sana ambazo unaweza kuzichagua. Kwa mfano Chrome Os inafanya kazi nzuri sana katika laptop za ChromeBook.
Sawa unaweza ukawa unafikiria kuwa labda chromeOs inaingia katika laptop za chromeBook tuu. Hapo awali ningesema uko sahihi, lakini kwa sasa kuna njia mbadala kuna program endeshaji (OS) inaitwa CloudReady ambayo inafanya kazi kama Chrome Os tuu.
CloudReady imetengenezwa na kampuni lijulikanalo kama Neverware, Os yao unaweza ukasema nit oleo tuu la Chrome Os lakini Os hii inatumiaka katika laptop na desktop nyingi zaidi na tofauti tofauti.
Cha furaha zaidi ni kwamba Os hii ni bure kwa matumizi ya nyumabani (yale ya kawaida tuu). Kushusha na Kupakua Os mpya ya CloudReady sio shida japokuwa wengi tunajua kuna ujanja ujanja wa kufanya hapa. Lakini kampuni la NeverWere limetoa hapa stepu moja hadi nyingine za kufuata wakati wa kuweka Os hiyo katika kompyuta yako.
Kwa kifupi CloudReady inafanya kazi kwa Laptop na Desktop ambazo zimetengenezwa kuanzia mwaka 2007 na kuendelea kutokana na repoti iliyopo. Inahitaji japokuwa GB 1 ya RAM ili ifanye kazi kwa ufasaha, lakini kwa kuwa inategemea sana uhifadhi wa mtandaoni (Cloud Storage) na utumiaji mwingi wa App za mtandaoni basi inahitaji GB 8 tuu za uhifadhi
Kama unahisi wakati unabadilisha kwenda katika OS ya CloudReady hii utapoteza vitu au taarifa zako za muhimu ondoa shaka kwani unaweza ukaweka mafaili yako katika Drive, picha zako katika Google Photos na kuweka muziki wako katika Google Music. Ukishamaliza kupakia Os yako katika kompyuta unaweza ukayashusha mafaili yako. Pia kama utapenda kutumia DropBox pia unaweza ukafanya hivyo.
Ukitumia njia hii lazima upate raha ukiwa unatumia kompyuta yako ya zamani. Pia sio lazima utumie Os Hizi mbili tuu naamini kuna Os nyingi sana hata mia zinaweza zikafika cha msingi ni kupata ile ambayo utaipenda.
Kama unahisi utapata shida au unapata shida juu ya namna ya kuweka programu endeshaji hizi katika kompyuta yako ni vizuri ukampatia mtaalamu afanye zoezi zima
OS = Programu Endeshaji