fbpx

NASA: Mwanamke ndio kuwa mtu wa kwanza kutua Mars (Mihiri)

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kiongozi wa juu katika taasisi inayojihusisha na utafiti wa masuala ya anga nchi Marekani NASA amesema kwamba mwanamke ndio anauwezekano mkubwa kuwa mtu wa kwanza kutua Mars (Mihiri).

Rais wa NASA Jim Bridenstine, aliyasema hayo alipokuwa kwenye kipindi kimoja cha redio. Sayari ya Mihiri ni moja ya sayari ambayo NASA wamewekeza utafiti mwingi kwa ajili ya kugundua chanzo cha maisha, kama kulishakuwaga na viumbe hai katika sayari hiyo na pia kama kuna uwezekano wa kuiegeuza sayari hiyo kuwa koloni huko mbeleni.

mtu wa kwanza kutua Mars

Mtu wa kwanza kutua Mars : Mfumo wa sayari, Mars ikiwa tuu baada ya dunia

Bridenstine alisema bado haijaamuliwa rasmi ni mtu gani ataenda katika sayari ya Mars, lakini alisema kwamba mipango yao kwa siku zijazo ni kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu na kuwa mstari wa mbele.

INAYOHUSIANA  Misheni ya Juno : Mambo yote ya kuyajua kuhusu Safari hii ya NASA

Bridenstine, alimjibu shabiki mmoja aliyemuuliza kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kama katika safari ya mwezi ujao ya NASA kutakuwa na nafasi kwa wanawake , kwa kusema “bila shaka”

Shirika la NASA linachukua hatua mbalimbali kuongeza ushirikishwaji wa wanawake katika maeneo ya kitafiti ya shirika hilo. Wafanyakazi wanawake wa mambo ya anga wenye uwezo wa kwenda anga za mbali (astronauts) wanamefikisha asimilia 34 ya timu nzima.

filamu sayari ya mars

Baadhi ya filamu maarufu kuhusu binadamu kufika Mars

Inasemekana kwa sasa ukitazama filamu/muvi nyingi za mambo ya anga hasa hasa kwa binadamu kufika Mars, nyingi zinampa mwanaume nafasi ya mtu wa kwanza kutua Mars. Kutokana na hili la NASA labda muvi zijazo zitaanza kuwa tofauti.

Vipi je una mtazamo gani juu ya uamuzi huu wa NASA wa kutoa vipaumbele kwa wanawake zaidi?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.