Inaweza ikawa hatuwezi kujitumia ushauri kwa matendo yetu mabaya tuliyofanya zamani lakini teknolojia imefanya tuweze kujitumia barua pepe katika miaka kadhaa ijayo
Barua pepe hii sio lazima itufikie sio bali tunaweza hata kuwatumia watu wengine mbalimbali. Usije ukashangaa mtu katangulia mbele za haki miaka kadhaa iliyopita alafu unapokea barua pepe yake.
FutureMe.Org ndio iko nyuma ya mchezo wote, huduma hii inafanya kazi kama huduma zingine za barua pepe. Cha muhimu ni kwamba inataka uweke tarehe kamili ambayo unataka barua pepe hiyo iwasili.
Barua pepe ambayo inatumwa inaweza ikawa inahusiana na mambo mengi, inaweza ikawa inatoa angalizo, ushauri, onyo au ikawa tuu inatoa salamu kutoka kipindi cha nyuma.
Kampuni imesema kupitia huduma yake mtu unaweza ukajitumia maneno ambayo yanaweza yakakutia nguvu katika jambo Fulani. Ukiachana na hili kuna mambo mengine mengi mazuri yanaweza yakafanyika kutokana na huduma hii
Kingine cha muhimu katika mtandao huu ni kwamba unashauriwa kutumia anuani ya barua pepe yako ya Gmail au mtandao mwingine lakini piga uwa isiwe na kazini kwako. Kumbuka miaka kadha tokea sasa unaweza ukawa umeshaiacha kazi hiyo
Mtandao unakuruhusu kutuma barua pepe hiyo kwa usiri mkubwa na pia unaweza hata ukaficha utambulisho wako
Kutokana na sababu za kisheria ni kwamba mtandao huo umepiga marufuku kwa watumiaji wake kuwataja majina watu ambao watakuwa katika barua pepe hiyo itakayotumwa. Kama umesajiliwa katika mtandao huo unaweza pia ukamtumia mtu mwingine – ukiachana na wewe mwenyewe – barua pepe
kuingia katika mtandao bofya – https://www.futureme.org/