Je ushasikia au kuona sehemu kuhusu teknolojia ya Microsoft Azure? Ni nini hasa? Hii makala fupi itakusaidia kufahamu.
> Microsoft Azure ni nini?
Microsoft Azure ni huduma ya mfumo wa kiteknolojia ya ‘cloud’ kutoka Microsoft inayowezesha pia huduma na teknolojia mbalimbali kama vile ‘analytics’, computing, database, masuala ya ‘networking’, diski uhifadhi (storage) na huduma zingine za kimitandao yaani Web.

Kupitia Microsoft Azure apps zinaweza tengenezwa na kusambazwa vyote vikiweza fanyika kupitia mfumo wa teknolojia ya Cloud.
Katika eneo la usalama kama ilivyo kwa huduma zingine za kimtandao mfumo mzima wa Microsoft Azure unalindwa dhidi ya wadukuzi – ‘hackers’.
> Je unafahamu tunaposema teknolojia ya Cloud tunamaanisha nini?
Kama umekwishatumia app na huduma kama vile za DropBox, Google Drive na nyingine kama hizo basi fahamu ya kwamba tayari umetumbia huduma za teknolojia ya Cloud. Teknolojia ya cloud inakuwezesha kutumia huduma mbalimbali za kikompyuta kupitia intaneti huku ikikuwezesha kutumia nguvu (nafasi) ya kompyuta nyingine kupitia huduma husika unayotumia.
Mfano; unaposave kitu kwenye DropBox au OneDrive basi fahamu ya kwamba kuna kompyuta flani inayomilikiwa na DropBox ndio umeitumia kuhifadhi mafaili hayo.
> Teknolojia ya Cloud
Teknolojia ya Cloud imekua sana kwa sasa na kupitia teknolojia hiyo kuna mambo mengi sana yanawezekana kufanyika nje tuu ya huduma kama vile za kuhifadhi mafaili (storage) na huduma ya Microsoft Azure ni mfano tuu wa kukuonesha ni mangapi yanawezeshwa kupitia teknolojia ya Cloud.
Kupitia teknolojia ya Microsoft Azure kuna huduma mbalimbali zinawezekana; kuanzia kwa watumiaji wa kawaida hadi kwa ‘developers’, yaani watengenezaji mitandao na apps.
> Kwenye huduma za Microsoft
Microsoft wameunganisha huduma za programu/apps zao mbalimbali na huduma za Azure. Mfano huduma kama vile za Microsoft 365, Bing, Microsoft Dynamics, OneDrive, Skype na Xbox Live zote zimewezeshwa (intergrated) pia teknolojia ya Azure katika mifumo ya intaneti.
> Kwa Developers
Watengenezaji apps na huduma zingine za kimtandao wanaweza kutumia Azure katika utengenezaji wao wa applications zozote. Watengenezaji apps wataweza kupitia Azure kutengeneza na ‘kudeploy’ applications zao kwa watumiaji wa programu endeshaji (OS) za Windows, Android na iOS.
Pia kupitia mifumo uandishi ya kimpyuta (code) kupitia huduma ya Azure Microsoft wanahakikisha programu zote zinazotumika katika utengenezaji wa applications zako zinakuwa updated na unatumia toleo jipya zaidi mara zote. Pia kuna huduma zingine kama vile ‘automatic backups’ n.k zote zikiwa kwenye mfumo wa Cloud.
> Kwa biashara/makampuni
Kwa makampuni na biashara ambazo tayari zinatumia huduma za Microsoft kama vile Dynamics CRM, Dynamics AX, NAV au GP kuhamia kwenye huduma ya Azure kunaleta faida katika gharama na ufanisi.
Pia huduma ya Azure inawapa nafasi watu wanaoitaji kazi za kufanywa na kompyuta yenye nguvu sana – kama vile usomaji wa data kubwa sana au kufanyia kazi (decode & encode) mafaili makubwa ya video, kutumia kompyuta kubwa zenye uwezo mkubwa kupitia huduma Azure. Kazi hizo zitakamilishwa kupitia mfumo wa Cloud.
> Je ni bora kuliko huduma za Cloud za Google na Amazon?
Hili linategemea mengi ila haraka haraka Microsoft wanahuduma nyingi sana zinazotumiwa na wengi kila siku na zote zinaweza kutumiwa kwa unafuu na ufanisi zaidi kutokana na huduma hizo kuna na uwezo wa Azure.
Katika masuala ya datacenters (vituo vya kompyuta data) Microsoft wanamiliki vituo hivyo katika maeneo 22 duniani, hii ni kiasi kikubwa sana ukilinganisha na Google Cloud au Amazon Web Service – wapinzani wao.
Je ulikuwa unafahamu kuhusu Microsoft Azure kabla? Tuambie kwenye ‘comment’
Vyanzo: Microsoft.com na vyanzo mbalimbali