Kwa baadhi ya maeneo kama Tanzania mitandao ya picha na video za kingono yamefungiwa, kwa sisi ni wazi mtandao kama vile Pornhub umefungiwa sio? Lakini ilikua ukiingia katika kurasa zake katika mitandao ya kijamii unona vitu wanavyotuma humo.
Kila mtandao wa kijamii una vigezo na masharti katika utumiaji wake sio? Hayo ni mambo ambayo pengine ukiyakiuka ni lazima watachukua hatua dhidi yako.
Katika hatua hizo, moja wapo ni kukufungia kwa muda au kukufungia kabisa. Kingine cha kuzingatia hapa sio lazima akaunti yako ya mtandao wa kijamii iwe ni ile ya kingono au vitu kama hivyo.
Hapa ni kwamba akaunti yeyote (hata ya kanisa au msikiti) ikiwa inakiuka vigezo na masharti ni lazima ichukuliewe hatua.
Wiki iliyopita mambo yalizidi kuwa mabaya kwa kampuni ya Pornhub baada ya akaunti yao ya Instagram kufungiwa kabisa na Meta.
Meta ndio wamiliki wa makampuni ya Instagram, Facebook na WhatsApp, na sababu ambayo wameitoa ambayo imewapelekea kuifuta akaunti hiyo ni ukiukwaji wa sera na sio mara moja jambo hili limejitokeza.
Kwa kipindi cha miaka kumi, Meta idai kuwa pornhub imekua ikikiuka huduma yake katika maudhui ya kikubwa, na maswala mengine yanayohusisha utupu.
Ukaichana na hiyo ni kwamba kampuni haijaweka wazi wazi kabisa kwamba sera hizo zimekiukwa kwa namna gani?
Wao Pornhub wamesema wameonewa na wamekwenda kulalamika kupitia ukurasa wao wa Twitter
Kingine ni kwamba maudhui ya namna hii huwa yanapotosha sana jamii na kuna umri fulani ambao inabidi kutazama maudhui haya na vile vile hayapaswi kutazamwa kwa namna stahiki – hivi ni moja kati ya vitu ambavyo vikikosekana huleta shida
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment je hili unalionaje? Je jambo hili ni sawa au unahisi kampuni ya pornhub inaonewa tuu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.