fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Intaneti Maujanja

NYWILA au Password: Vitu Muhimu vya Kufahamu na Kuzingatia. #Usalama

Je ni mambo gani muhimu ya kuzingatia katika kutengeneza Password a.k.a nywila iliyo salama zaidi? Leo tutakufundisha jinsi ya kufanya hivyo.

Nywila ni neno sanifu la Kiswahili kwa ajili ya neno “Password”. Maneno mengine ambayo hutumika kwa umaarufu zaidi ni kama Nenosiri na Neno la Kificho.

Je ni mambo gani muhimu ya kuzingatia katika kutengeneza Password

Je ni mambo gani muhimu ya kuzingatia katika kutengeneza Password a.k.a nywila iliyo salama zaidi? Epuka utumiaji wa namba zinazoendana au maneno yanayotengeneza maana

 

Hii ni moja ya njia za kuweka usalama katika taarifa mbalimbali katika mifumo ya kielektroniki kupitia simu , tarakilishi (kompyuta) ama vifaa vyovyote vya kielektroniki vyenye uwezo wa kufungua taarifa hizo.

SOMA PIA  Machapisho ya picha na video kuweza kuweka muziki

Mifumo mbalimbali ya kielektroniki huwa na vigezo ambavyo vimewekwa kwa ajili ya utengenezwaji wa Nywila. Vigezo hivi huwa na uhusiano toka mfumo mmoja hata mwingine maana ni njia ya kuweka ulinzi ambayo ni maarufu na hutumika zaidi. Baadhi ya vigezo hivyo ni.

  1. Lazima iwe na herufi zisizopungua sita (6), ama nane (8), kutegemeana na mfumo.
  2. Lazima iwe na mchanganyiko wa herufi (A-Z), tarakimu (0-9), na alama mbalimbali.kama #,+ n.k..
  3. Kuwa na mchanganyiko wa herufi kubwa na ndogo.
SOMA PIA  Wiki mbili za ziada kwa watumiaji wa WhatsApp kwenye Blackberry 10 OS

Vigezo hivi ni vya msingi katika kuimarisha usalama wa nywila yako kutambulika na wewe binafsi , hivyo kuifanya kuwa salama na ngumu kwa mtu mwingine kuidukua.

Nia kuu ya Nywila ama Nenosiri ndio faida yake kuu pia. Nayo ni kuweka ulinzi wa taarifa za mtu binafsi, kikundi cha watu, taasisi ama shirika zilizo katika mfumo wa kielektroniki.

Kwa sababu nywila huweza kubeba mchanganyiko wa herufi, tarakimu na alama mbalimbali, hii humaanisha uwanja mpana wa uchaguzi wa nywila ili kutokuwa rahisi kwa mdukuzi.

Pamoja na hayo, kuna hatua mbalimbali za kiusalama za kuchukua ili kuhakikisha usalama binafsi wa nenosiri lako, ikiwemo.

  1. Kubadilisha nywila ama nenosiri kila baada ya siku 90 (miezi mitatu)
  2. Kutowashirikisha nywila yako watu wengine kama marafiki na watu wa karibu.
  3. Kufunga akaunti ama mfumo wenye taarifa zako (logging out) mara baada ya matumizi, hasa ukiwa ulifungua kwenye kifaa kisicho chako.
  4. Kutokutumia nywila sawa katika mifumo/huduma mbalimbali, maana ni hatari. Endapo itadukuliwa, mifumo yote itakosa usalama
SOMA PIA  Matumizi 5 Ya Kamera Ya Simu Janja! #Maujanja

Soma Makala zingine zinazohusu Maujanja ya kwenye Simu na Kompyuta -> Teknokona/Maujanja

Ni muhimu kuandika nywila zako za mifumo mbalimbali mahali ama kutumia programu na mifumo ya utunzaji wa nywila kama mfumo wa Google ili kutunza nywila yako.

Joshua Maige

Mkazi wa Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa sasa, ni mwanafunzi katika Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam(DIT), pia ni mwandishi wa makala za kiteknolojia katika ukurasa wa Teknokona.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania