fbpx

Jifunze kutengeneza mafaili ya GIF kupitia WhatsApp

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Jifunze jinsi ya kutengeneza mafaili ya GIF kupitia WhatsApp na kuweza kutuma kwa ndugu au marafiki kwa urahisi bila uhitaji wa app nyingine.

WhatsApp ni moja ya App inayoongoza kwa kuwa na watumiaji wengi zaidi duniani. Katika siku za karibuni imekuwa ikiendelea kufanya maboresho yanayokidhi haja za wengi.

Moja maboresho mazuri ni kumuwezesha mtumiaji wake kutengeneza mafili ya GIF bila ya kutumia programu maalum ya kufanya hivyo.

kutengeneza mafaili ya GIF kupitia WhatsApp

Kutengeneza mafaili ya GIF kupitia WhatsApp

Leo tutakufahamisha namna ya kutengeneza mafaili ya GIF kutoka katika video yoyote uliyonayo katika simu yako. Tutakuwekea maelezo mafupi kisha picha itakuonesha kwa urahisi namna ya kutengeneza mwenyewe. 1.Fungua WhatsApp yako na uende kwenye namna ya unayemkusudia kumtumia

INAYOHUSIANA  Unamfuatilia kisiri mtu Instagram? Instagram wafanya iwe vigumu!

2.Bonyeza icon ya Attachment

3.Chagua Gallery

4.Chagua video ambayo unataka kubadili kuwa GIF.

5.Weka sehemu ya Video unayotaka iwe faili la GIF (Ni vizuri faili lisizidi sekunde sita)

Angalizo: Kuna baadhi ya simu namba nne na namba tano zinakuwa tofauti. Yaani unaanza hatua ya tano kisha hatua ya nne ndio unapata chaguo la kuweka GIF.

6. Tuma kwa mlengwa faili lako la GIF

INAYOHUSIANA  Utaweza Kubackup Kompyuta Nzima kupitia Google Drive

Bila shaka umependa somo la leo.

Je una lolote la kutuambia au kushauri. Video yako ya kwanza kutengeneza faili la GIF wadhani itakuwa ni ipi? Tutumie maoni au ushauri wako hapo chini katika sehemu ya maoni.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.