Je?! wewe ni mmoja kati ya watu ambao wanakesha wakiangalia video ama makala katika mtandao wa Youtube kila siku?!, kama jibu ni ndiyo basi unajua jinsi ambavyo mwanga wa kompyuta huwa unachosha ama kufanya macho kuuma.
Makala hii itakuelewesha namna ya kuwasha Nightmode ya Youtube ili kutumia toleo maalumu la mtandao huu kwaajiri ya nyakati za giza ama mwanga hafifu.
Night mode ya mtandao huu kwa imekuwapo kwa miezi kadhaa sasa na kama unataka kuitumia basi unahitaji kufuata hatua zifuatazo;
- Fungua ukurasa wa Youtube katika browser yako
- Ingia katika akaunti yako
- Fungua “development tools” kama unatuia OS ya windows basi una bofya Ctrl + Shift + I ama Option + Command + I kama unatumia kompyuta za Mac
- Bofya sehem iliyoandikwa “console”
- Nakili code ifuatayo:- document.cookie=”VISITOR_INFO1_LIVE=fPQ4jCL6EiE” katika sehemu ya kuandika kisha bonyeza enter
- Funga “development tools” halafu Refresh ukurasa wako na kisha ingia tena katika akaunti kama zoezi hili limekutoa katika akaunti
- kuwasha nightmode bofya katika kipicha cha akaunti yako ya youtube na kisha nenda katika nightmode.

Tayari baadhi ya mitandao kama Twitter imekwisha leta uwezo wa kutumia Nightmode katika app zao za simu, haitakuwa jambo la kushangaza iwapo Youtube pia watafanya hivyo.