Huwezi ingia katika mtandao kwa lengo lakutafuta kitu bila kutumia kivinjari (browser) chochote. Vivinjari hivi vipo vya aina nyingi sana inategemea tuu na matumizi yako.
Kwanza kabisa kabla ya yote ni kivinjari (browser) gani unachotumia kusoma hii makala? Kama unatumia kivinjari kilichokuja kabisa na kompyuta kama vile Internet Explorer katika Windows au Safari katika Mac inakubidi ukuze machaguo yako.
Kuna vivinjari ambavyo unaweza ukavipenda zaidi kwani vinaweza vikawa na vipengele vingi zaidi kwa mfano katika usalama, muonekano n.k.
Sasa ni kivinjari kipi ambacho kipo kwa ajili yako? Enndelea kusoma ili kujua kipi unakipenda kati ya hivi vichache vikuu. Unaweza ukashangaa chaguo lako linaangukia katika kimoja hapa.
GOOGLE CHROME
Watabiri walitabiri kuwa kivinjari hiki kitakipita kivinjari cha Internet Explorer (IE) kama kivinjari kinachotumika sana duniani. Pia kina vipengele vingi na vya aina yake ambavyo vinaweza vikakushawishi uhamie kwake. Pia kivinjari hiki kinaongelewa kama kivinjari ambacho kina spidi ya hali ya juu wakati mtu akitumia.
Chrome pia inaruhusu matumizi ya ‘Extensions’ mbalimbali ili mradi tuu ufurahie au ukidhi mahitaji yako vizuri wakati unakitumia. Pia unaweza uka ‘Sync’ bookmarks katika kompyuta yako kwenda katika Simu janja kwa kutumia App ya Google Chrome.
INTERNET EXPLORER
Kama wewe ni mtumiaji wa intaneti toka zamani ni lazima utakuwa unakijua hiki kivinjari. Tena labda bado unatumia IE tuu. IE ni kivinjari toka kwa Microsoft ambacho kimekua kikitumia toka enzi hizo.
Siku hizi vivinjari mbadala vya IE (kama vile Mozilla na Chrome) vimekuwa maarufu sana nah ii ni kutokana na utendaji wake mzuri wa kazi na kuwa na ulinzi wa juu kuliko IE. Na pengine ndio sababu Microsoft iliamua kuacha kutoa sapoti katika baadhi ya matoleo yake, na pia mwaka jana Microsoft ikazindua kivinjari kingine kinachoitwa Microsoft Edge.
MICROSOFT EDGE
Kivinjari hiki kilitoka spesheli kwa ajili ya matumizi ya kisasa ya kimtandao ambayo ni bora zaidi kuliko IE. Juu ya hilo ni kwamba inafanya kazi nyingi sawa na Mozilla na Chrome. Kivinjari hiki kimetengenezwa spesheli kwa programu endeshaji ya Windows, Yaani Microsoft Windows 10.
Japokuwa Edge ina mapungufu kidogo, matatizo katik asalama na uhaba wa ‘Extensions’ bado kuna sababu kibao tuu za kujiunga na kivinjari hicho.
Edge pia inafunga mitandao haraka zaidi kuliko kivinjari kingine chochote na pia hata kama unajihisi umechoka au huwezi kuandika unaweza ukatumia kivinjari hicho kwa kuongea tuu kupitia Cortana.
MOZILLA FIREFOX
Hiki ni kivinjari kingine ambacho kina spidi nzuri tuu na kina ulinzi mzuri tuu. Kinafahamika kwa kuruhusu watumiaji kuongeza mambo mabalimbali katika kivinjari hicho. Kuna zaidi ya programu 100,000 ambazo zinamsaidia mtumiaji wakati akiwa anakitumia.
Pia kivinjari hiki kina matoleo ya Kompyuta na hata yale ya simu ambayo watu wanaweza wakatumia. Pia Mozilla mara kwa mara inajisasisha (update) kwa hiyo haina haja yaw ewe kufikiria sana kuhusu hilo, na pia ikifanya hivyo inamaanisha hata ulinzi utakuwa unaimarishwa zaidi.
OPERA
Kivinjari cha Opera kipo kwa miaka mingi sana lakini cha kushangaza kipo nyuma sana kwa kulinganisha na vivinjari vingine. Opera kina uwezo wa kufuatilia vizuri katika usalama kutokana na ‘Software’ hatarishi. Pia ina spidi nzuri tuu, lakini kubaki nyuma kwake ni aibu sio? Maana nna uhakika kinatumiaka sana kwenye simu za watu (tena hasa simu ndogo ndogo), kwenye kompyuta kinatumika kwa kiasi kidogo sana.
Kutokana na hayo yote wewe kama mwana Teknolojia inabidi uchague kimoja cha kutumia – au umeshachagua? – Taarifa zilizopo ni kwamba kivinjari cha Google Chrome ndio kivinjari kinachotumiwa kwa sana duniani kuliko kingine chochote. Kama unataka kuwa kama wengi linaweza likawa ndio chaguo lako