Kama una iPad au iPhone na unataka kuficha App fulani ili mradi isionekane katika skrini bila ku ‘JailBreak’ hilo linawezekana.
Kama inavyojulikana wengi wanafaidi kutumia vifaa vyao vya iOS (iPhone na iPad) kama wakive ‘jailbreak’. Ukifanya hivyo unakiruhusu kufanya vitu vingi ambavyo visingiweza patikana katika hali ya kawaida. Kwa mfano kuna App mbalimbali ambazo zinapatikana pindi tuu unapo ‘JailBreak’ simu yako bila kufanya hivyo hautaziona katika soko la ‘AppStore’.
JINSI YA KUFANYA HIVYO
- Kwanza kabisa itoe App unayotaka kuificha na ipeleke katika folder lililopo au kama unapendelea tengeneza jipya. Ukitaka kuhamisha App hiyo bonyeza App hiyo bila kuiachia mpaka App zote zianze kucheza cheza, hapo sasa unaweza ishikilia na kuihamisha mpaka kwenye ‘Folder’ hilo.
- Ukishafanikiwa kuihamisha App hiyo, hakikisha unaiweka App hiyo sehemu ya mwisho kabisa katika folder yani isiwe na app zingine upande huo wa folder (kama kuna App, ipeleke App hiyo kurasa ya mbele ya folder hilo). Kufanya hivyo rudia kushika App hiyo mpaka zingine zote zianze kucheza cheza na kisha ihamishe mpaka eneo la mwisho
- Ukishapeleka App yako katika ukurasa wa mbele tofauti na App zingine, bila kuiachia bofya kitufe cha nyumbani (home) katika kifaa chako
- Kwa kufanya hivyo utashangaa kuona App yako imepotea katika skrini ya kifaa chako.
Ukifanya hivyo unaweza ukaipata App yako tena katika eneo la tafuta (search) ukifika pale cha kufanya ni kuandika jina la App hiyo
Hii inawafaa sana wale ambao wana App ambazo hawapendi zionekane kwa watu wengine. Na pia kuna baadhi ya App kama vile WhatsApp ambazo zinakuwa na taarifa mbalimbali za mtu. Kama hutaki zionekane na unatumia iDevice hii inaweza ikawa ya msaada kwako.
Kwa maelezo ya vitendo zaidi, tazama video fupi upate kujionea mwenyewe.