fbpx

Kampuni Ya Ujerumani Kuweka Mnara Wa Simu Mwezini!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Ni vigumu sana kuwasiliana na mtu ambaye yupo mwezini sio? Lakini hili linaweza likabaki kuwa historia kwani kwa sasa kampuni kutoka ujerumani iko katika mchakato wa kuliwezesha hilo.

Kampuni kutoka ujerumani inayojulikana kama Part Time Scientists (PTScientists) ndio ambayo inafanya mchakato mzima wa kuhakikisha kuwa mpaka ifikapo 2018 kutakuwa na uwezekano wa mawasiliano kutoka mwezini hadi duniani.

Hili litawezeshwa kwa kuweka mnara wa simu katika mwezi hivyo basi kwa msaada wa teknolojia ya LTE, uwezekano wa mawasiliano baina ya pande mbili unaweza ukafanikiwa.

Magari Ambayo Huenda Yakatumika Katika Teknolojia Hii

Ili kutumia teknolojia ya LTE kampuni limeamua kuingia katika ushirikiano na kampuni kubwa katika maswala ya mawasiliano linalojulikana kama Vodafone.

Ukiachana na Vodafone bado kampuni ipo katika ubia na kampuni ya magari ijulikanayo kama Audi.

Kwa haraka haraka ni kwamba minara hiyo itakua ikitembea katika uso wa mwezi, yaaani kupitia vigari (vidogo kabisa)kutoka Audi yatakua yamebeba mitambo mithili ya mnara wakati Vodafone wakitoa teknolojia ya LTE.

Jambo hili linaungwa mkono kutoka pande nyingi sana hebu fikiria kuwasiliana moja kwa moja na mtu ambaye yupo mwezini. Tofauti na zamani ambapo ilinibidi mtu asubirie stori kutoka kwa mtu huyo akirudi duniani.

Video Ikionyesha Audi Wakieleza Sababu Zao Kuungana Na PTScientists Na Kwenda Mwezini.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment. wewe hili umelipokeaje kumbuka kuwasiliana kutoka mwezini sio mchezo?

Tembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila SIku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.