fbpx

Anga, NASA, SpaceX

Nasa na SpaceX: Wafanikisha safari ya kwanza ya wanasayansi iliyohusisha kampuni binafsi. #Anga

nasa-na-spacex-safari-ya-kwanza-wanasayansi-anga

Sambaza

Jumamosi imeweka rekodi kubwa katika sekta ya safari za anga za juu. Nasa na SpaceX walifanikisha safari ya kwanza ya wanasayansi kwenda anga za juu kupitia ushirikiano wao.

nasa na space x
SpaceX (Space Exploration Technologies Corp) wamekuja na teknolojia nzuri katika sekta ya anga.

 

Hii ni mara ya kwanza kwa kifaa kilichotengenezwa na kumilikiwa na kampuni binafsi kupeleka wanasayansi katika kituo cha kimataifa cha angani (International Space Station).

SpaceX ni kampuni iliyoanzishwa na Elon Musk mwaka 2002 ikiwa na lengo la kushusha gharama za safari za anga na pia kuwezesha safari za kwenda kwenye sayari ya Mirihi / Masi. Hii ndio kampuni ya kwanza binafsi kupeleka mizigo kwenye kituo cha anga cha kimataifa na pia kwa sasa imekuwa ndiyo ya kwanza kupeleka wanasayansi kwenye kituo hicho pia.

Kwa nini SpaceX wametumika?

Ni zaidi ya miaka nane sasa tokea NASA (Shirika la Serikali ya Marekani linalohusika na utafiti wa anga) kupeleka watafiti/wanasayansi wake kwenye kituo hicho cha anga kwa kutumia chombo chake chenyewe. Kwa muda mrefu wamekuwa wakiwategemea Urusi kwenye usafirishaji wa wanasayansi wao kwenda kwenye kituo hicho cha anga, na wamekuwa wakiwalipa pesa nyingi.

nasa na spacex
Roketi zikirudi na kusimama ardhini baada ya kutumika

SpaceX wamekuja na teknolojia inayowaruhusu kutumika tena kwa vifaa vyao vya usafirishaji (roketi). Kutokana na teknolojia hiyo wameweza kushusha sana gharama za uendeshaji. Teknolojia ya rokoti inayotumiwa na Urusi na ata NASA inahusisha kutoweza kutumika tena kwa rokoti baada ya kuruka – huwa zinachomoka zikifika anga za juu na hivyo kuharibika / kuungua baada ya utumiaji.

INAYOHUSIANA  Marekani kuzidisha katazo la Laptop katika ndege za kimataifa

 

Kupitia ushirikiano huu na SpaceX, NASA wanategemea kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama za safari zake na pia ni jambo la sifa kwa taifa la Marekani kwa kutokuwa tegemezi kwa huduma za Urusi.

wanaanga nasa
Wanaanga wawili wa NASA (waliovaa suruali za khaki) baada ya kufika kwenye kituo cha kimataifa cha anga.

 

Gharama za safari kwa kuwatumia SpaceX ni takribani robo ya gharama ya safari hiyo hiyo kwa kutumia mashirika mengine ya anga.

Je unadhani lengo lao la muda mrefu la kufika Mirihi / Masi na kuanzisha makazi litafanikiwa? Wengi wanaamini kwa kasi hii ya maendeleo hilo pia litaweza kufikiwa, ni suala la muda tuu.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |