fbpx

Anga, Ndege, SpaceX, Usafiri

Jaribio la Starship: SpaceX wafanikiwa kurusha chombo cha anga cha safari za mbali za anga

jaribio-la-starship-spacex-wafanikiwa

Sambaza

Jaribio la Starship lafanyika kwa mafanikio wiki hii. Starship ni ndege spesheli kwa ajili ya safari za anga kati ya sayari yetu na mwezi, au sayari yetu kwenda sayari nyingine inayotengenezwa na kampuni ya SpaceX ya nchini Marekani.

Ndege hiyo iliyo kwenye mfumo wa roketi za anga, ilifanyiwa majaribio kutoka kiwanda cha SpaceX kilichopo kwenye mji mdogo wa Boca Chica katika jimbo la Texas nchini Marekani. Ina urefu wa zaidi ya mita 10 kwenda juu.

jaribio ya starship
Jaribio la Starship: Ndege-roketi ya Starship ikiruka kutoka kituo cha utengenezaji na utafiti cha SpaceX, mji wa Boca Chica nchini Marekani.

 

Ingawa majaribio haya yanachukuliwa kama ni majaribio yaliyokuwa na mafanikio makubwa chombo hicho cha anga kilishindwa kutua, kilifika hadi eneo la kujua ila mwendo ulikuwa ni wa kasi sana na hivyo kililipuka na kuharibika kabisa.

starship
Starship
  • Ndege/Roketi hiyo iliweza kupaa umbali wa kilometa 12,500 juu ya uso wa dunia kabla ya kujirudisha chini kwa ajili ya kutua.
  • Ikiwa angani iliweza kujigeuza kutoka kutazama juu, na ikakaa ikiwa inatazama pembeni. Ikiwa katika mkao huo iliweza kuchezesha mabawa yake ili kuweza kujipeleka usawa sawa. Hii ni kwa ajili ya majaribio ya kupunguza kasi ya kushuka chini kifaa hicho kitakapokuwa kinaingia kwenye anga ya dunia. Kupunguza mwendo kwa njia hii kunakipa uwezo mzuri wa kupunguza hali ya joto dhidi ya misuguano yake na anga wakati kikiwa kinaingia kwenye anga ya dunia kwa kasi kubwa.maribio ya starship spacex anga
  • Kupitia maneno ya Elon Musk, mlipuko huo ni kutokana na injini kutopata mafuta ya kutosha kwa kuwa tenki lilipungua ujazo – pressure, na hivyo kufanya injini zake kutokuwa na nguvu ya kutosha ya kupunguza kasi kipindi cha kutua.
SOMA PIA  FastJet kupata ndege mpya, Embraer E190. Ifahamu Zaidi

 

SpaceX wanasema kuweza tuu kufanikiwa kupaisha ndege hiyo hadi juu na kuweza kuirudisha salama hadi eneo la kutua ni mafanikio makubwa kwao. Lengo lao kuu lilikuwa kuweza kupata data zaidi juu ya ubunifu na teknolojia zao ili kuweza kuboresha zaidi katika ndege zingine ambazo tayari zipo tayari kwa majaribio mengine.

SOMA PIA  Uwezo wa kuwagawa washiriki kwenye makundi ndani ya Google Meet
Jaribio ya Starship
Mlipuko wa Starship wakati wa kutua

Kupitia Starship kampuni ya SpaceX chini ya uongozi wa Elon Musk inataka kutengeneza chombo cha usafiri kitakachorahisisha:

  • Safari za anga kati ya sayari yetu na sayari zingine
  • Safari za duniani pia, kwani Space Ship inaweza kufanya safari za umbali wa hadi masaa 8 – 12 za ndege za kawaida ndani ya muda wa lisaa limoja tuu.

Mafanikio ya Elon Musk kama mkurugenzi wa kampuni ya Tesla pamoja na kampuni ya SpaceX kumempa mafanikio makubwa na sifa nyingi ulimwenguni kote. Kwa mwaka huu tuu utajiri wake umekua maradufu na sasa ni mtu wa pili duniani kwa utajiri.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Comrade Mokiwa

Comrade MokiwaMuanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COMMuda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.| mhariri@teknokona.com |

Toa Maoni

Your email address will not be published. Required fields are marked*