fbpx
Mtandao wa Kijamii, Twitter

Twitter Kuja Na ‘Tweet Scheduling’ (Tweet Sasa Na Ipande Baadae)!

tweet-scheduling-ndani-ya-twitter
Sambaza

Twitter imeongeza kipengele ambacho kinajulikana kama ‘Tweet Scheduling’ ambacho kina maana ya kuwa mtumiaji wa twitter unaweza uka’tweet kitu lakini kitu hicho kikapanda katika ukurasa wake kwa muda wa mbele kabisa ambao utakua umeuchagua yeye.

Ni wazi kuwa hapo zamani kitu hiki kilikua kinashindikana kabisa kwa kutumia akaunti kuu na App ya twitter.. kuwezekana kufanyika kwa hili ilikua ni lazima kutumia App mbadala kama vile TweetDeck.

INAYOHUSIANA  SIGNAL: Facebook Waja Na Kipengele Kipya Kinachosaidia Waandishi Wa Habari!

Ukitaka kuwezesha kufanikisha hili hakikisha katika kompyuta (bila kutumia App) kisha ingia katika mtandao wa Twitter. Katika eneo la kuandika tweet kwa chini utaona kuina kialama cha kalenda. Ukiingia katika kialama hicho utakua na uwezo wa kuandika tweet unayotaka na kuiamuru iruke baadae kulingana na muda ambao wewe utakua umependekeza.

Jinsi Ya Ku'Schedule Tweet
Jinsi Ya Ku’Schedule Tweet

Najua swali ambalo unajiuliza hapo ni kwambi vipi kuhusu katika App zako za simu?. Kiukweli ni kwamba Twitter imekua ikihangaikia katika kufanya kipengele hiki kinawezekana kwa muda mrefu tuu sasa.

INAYOHUSIANA  Twitter waleta Stickers katika picha! #Apps

Hii inamaanisha kuwa watumiaji wa simu janja  wasubirie subirie maana siku za usoni kipengele hichi nacho wataanza kukipata katika simu zao.

Ningependa kusikia kutoka kwako, kumbuka TeknoKona daima tupo nawe katika swala zima la teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com