fbpx
Mtandao wa Kijamii, Teknolojia, TikTok, Uchina

TikTok kufungiwa Marekani: Muda umesogezwa mpaka siku 90

tiktok-kufungiwa-marekani-muda-umesogezwa-mpaka-siku-90

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Baada ya mafanikio makubwa ya haraka, TikTok wapo kwenye hatihati ya kufungiwa nchini Marekani. Je, sababu ni nini? Fahamu zaidi.

Kwa kipindi kirefu tangu kuchaguliwa kwa rais Donald Trump nchini Marekani taifa hilo limekuwa likiendesha kampeni kali inayoendana moja kwa moja na hatua za kisheria dhidi ya makampuni ya  Uchina huku wakiishutumu nchi hiyo na hatari za udukuzi wa kiserikali; yaani wakiamini teknolojia na bidhaa zinazotokea katika taifa hilo zipo kwenye uwezekano mkubwa wa kuwa na uhusiano wa kutoweza kunyima data binafsi za watumiaji wake zinapohitajika na serikali ya Uchina.

INAYOHUSIANA  NASA Waja na teknolojia mpya ya WiFi - Kutumia Chaji Kiasi Kidogo Zaidi

>Hapo awali kiongozi mkuu wa nchi nchini Marekani alikuwa ameipa zaidi ya mwezi mmoja za kuweza kusitisha kazi zake ama kuuza TikTok kwa kampuni nyingine au “Kujivua gamba” kutokana na kuwa tishio kwa sababu za kiusalama lakini amri hiyo sasa imebadilika na kuwa siku 90.

>Rais Trump anaamini kwamba kampuni hiyo inaweza ikapeleka taarifa za watumiaji wa Marekani na kuipa serikali ya Uchina kitu ambacho ByteDance imekataa na kusema wataendelea kuwaburudisha na kuwaunganisha wateja wake wanaofikia 100+ milioni kwa Marekani pekee.

Taarifa zinaeleza mwezi Aprili 2020 TikTok ikiwa imepakuliwa mara bilioni 2 lakini kutokana na misukosuko ambayo inakumbana nayo hadi kufikia mwezi jana ilikuwa imeshashushwa na watu 700 milioni duniani kote.

kufungiwa
Watumiaji wengi wa TikTok wanaonekana wapo nchini India ingawa takwimu hizi ni kabla ya kufungiwa.

Microsoft imeonyesha nia ya kutaka kununua TikTok na wanatazamiwa kutoa uamuzi wao mpaka kufikia Septemba 15 2020 ingawa Bw. Bill Gates haamini kama utakuwa ni uamuzi mzuri kuinunua iwapo wakifikia makubaliano.

Vyanzo: Deadline, The Verge

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|