fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Bitcoin Teknolojia

Historia ya Bitcoin

Historia ya Bitcoin

Spread the love

Historia ya Bitcoin. Kwa mara ya kwanza Bitcoin kuongelewa mtandaoni ilikuwa ni mwaka 2009 ambapo Satoshi Nakamoto alitoa andiko linaloelezea mfumo wa fedha za kidigitali unaojitegemea.

historia ya bitcoin

Historia ya Bitcoin

Alielezea kuwa “Kinachohitajika ni mfumo wa malipo ya kielektroniki kulingana na uthibitisho wa kielelezo badala ya uaminifu, kuruhusu vyama vyovyote vyenye hiari kushirikiana moja kwa moja bila kuhitaji mtu wa tatu anayeaminika”.

Bitcoin ilianza kupanda dhamani mwaka 2011 na baada ya hapo thamani yake ikawa inapanda taratibu, ilipofika mwaka 2014 thamani ya Bitcoin moja ikawa ni zaidi ya Shilingi Milioni 1. Mwaka 2017 thamani ya Bitcoin ikawa inapanda kwa kasi sana mpaka kufika Shilingi Milioni 34. Thamani ya Bitcoin ilishuka baada ya hapo kwa mwaka 2018 mpaka 2020 mwezi wa kumi ikaanza kupanda tena kwa kasi. Mpaka kufikia mwezi wa nne mwaka huu thamani ya Bitcoin moja ilikuwa ni sawa na Shilingi Milioni 142. 

Mfumo unaotumika kutengeza fedha hizi za kidigitali umeweka kikomo cha Bitcoin milioni 21 zinazoweza kutengezwa kwa mfumo huo, na kwa sasa tayari Bitcoin milioni 18 zimesha tengenezwa na zipo kwenye mzunguko.

Hadi sasa Bitcoin inatambulika rasmi kisheria kwenye mataifa mengi, hii ikiwa ni pamoja na; Marekani, Kanada, Uingereza, El Salvador, Afrika kusini, Mataifa ya Umoja wa Bara la Ulaya na mataifa mengine kadhaa. Kwa mataifa mengi ni kwamba imetambulika na si kosa kuitumia, ila kuitambua rasmi kutumika kwenye mifumo rasmi ya malipo ndilo jambo ambalo bado halijafanikiwa sana kwenye mataifa mengi. Bado vyombo vya kifedha vya mataifa mengi bado vinafanya tafiti ili kuweza kuielewa vizuri mifumo ya kiusalama katika mfumo huu mpya wa pesa za kidigitali.

SOMA PIA  Nokia 8110 yenye teknolojia ya kisasa

Marufuku!

Nchini Uchina, Bolivia, Columbia, Ecuador, na Urusi ni baadhi ya mataifa machache ambaye yanajaribu kuzuia utumiaji wa fedha hii ya kidigitali katika mataifa yao.

Endelea kufahamu mengi yanayoendelea kuhusu Bitcoin kwa kutembelea ukurasa wetu wa habari za Bitcoin hapa Teknokona/Bitcoin

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania