fbpx
simu, Smartphones

FUNUNU: Haya Ndio Yatakua Matoleo Ya Simu Janja Za Motorola 2017

fununu-haya-ndio-yatakua-matoleo-ya-simu-janja-za-motorola-2017
Sambaza

Simu Janja katika ulimwengu wa sasa ndio kila kitu! tunajua kwa kina kabisa kwamba zimerahisisha mambo mengi sana. Simu janja zipo za aina nyingi sana lakini leo tuangazie katika Motorola.

Motorola ni simu janja japokua wengi hawana muamko na simu hizi lakini pia usisahau kuwa hapo mwanzo simu hizi zilishawahi kuwa zinaongoza kwa mauzo duniani. Motorola ni kampuni ambayo bado inajikita katika kutengeneza simu janja nzuri kabisa

Kwa mwaka huu, fununu zilizopo ni kwamba kampuni itatoa simu za motorola katika matoleo matano. Hii inamaanisha kuwa  yatatoka matoleo mawili katika simu za mwendelezo wa  “C”, “E”, “G”, na “Z” na toleo moja katika mwendelezo wa simu za Motorola ‘X’. Leo TeknoKona itaongelea matoleo hayo juu juu tuu na yakitoka tutakupasha kwa undani zaidi.

INAYOHUSIANA  Kwa nini uchague au usichague simu za iPhone (iOS) badala ya Android?

Muendelozo Wa Motorola C

Hapa yatatoka matoleo mawili ambayo yanajulikana kama Moto C na Moto C Plus. Kila moja itakua na kioo cha inchi 5 japokua vioo hizo vitatofautiana ubora (resolution). Moto C ubora wa kioo chake utakua ni 480p wakati ule ubora wa Moto C Plus utakua ni 720p. Toleo la Motorola C lina hati hati kubwa ya kuja na betri lenye uwezo wa mAh 4000.

Muendelezo Wa Motorola G

Hapa tena yatatoka matoleo mawili ambayo ni Moto gs na Moto gS+ (Moto gs Plus). Toleo la moto gs litakuaja na kioo cha ubora wa FHD chenye inchi 5.2  wakati Moto gS inakuja na kioo cha ubora wa FHDchenye inchi 5.5. Moto gS+ inaweza ikaja na kamera mbili za nyuma wakati toleo la gS linaweza likija huku umbo lake lote likiwa limezungukwa kwa chuma

INAYOHUSIANA  Ijue simu mpya kutoka Motorola ya Moto Z3 Play
Matoleo Ya Simu Janja Za Motorola

Muendelezo Wa Motorola E

hapa kama kawaida yatakuja mengine mawili, Moto E na Moto E Plus. Moto E itakuja na kioo chenye ubora wa FHD na chenye inchi 5. Moto E Plus itakua na kioo kikubwa zaidi chenye inchi 5.5 na pia betri lake litakuwa na uwezo wa mAh 5000. Kingine kikubwa ni kwamba toleo la E Plus litakuwa na uwezo wa teknolojia ya alama ya kidole maarufu kama finger print kwa upande wake wa nyuma.

Muendelezo Wa Motorola Z

hapa pia yatakuja matoleo mawili, lakwanza kabisa likiwa ni Moto Z Play na Moto Z Force. Moto Z Play inakuja na kioo cha FHD chenye inchi 5.5. Taarifa za toleo la Moto Z Force kidogo hatuna kwa sasa. Tukipata taarifa nzuri kuhusiana na matoleo haya, utakua wa kwanza kujua.

INAYOHUSIANA  'Airtel Yatosha': Zawadi Bora Kwa Watanzania!

Muendelezo Wa Motorola X

Taarifa zilizopo ni kwamba hapa litatoka toleo moja tuu kwa mwaka 2017. Toleo hili la Motorola litakuja na kioo cha FHD chenye inchi 5.2. Kioo cha 3D na japokua hakuna taarifa nyingi kuhusiana na hii simu lakini pia inasemekana kamera yake itakua ni SmartCam.

Kwa mwaka huu haya ndio matoleo ya kuyasubiria kutoka katika kampuni ya Motorola. Simu janja hizi kwa haraka haraka zitakuwa ni za aina yake kwani kwa sifa chache hizi tuu zinaonyesha kwa kiasi gani zitakua ni nzuri

FHD = Full High Definition

Kwa taarifa kamili pale punde tuu zimu hizi zinapotoka, kaa karibu na mtandao namba moja katika maswala ya teknolojia ili usipitwe.

Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com