Unaweza ukawa na njia nyingi za kukuwezesha kufungua mafaili ya PDF kama katika kompyuta yako kama vile kwa kutumia mtandao, programu za kusoma mafaili katika mfumo wa PDF (PDF reader) na hata njia hii hapa. Ukiachana na njia hizo zote ipi rahisi sasa? Leo Teknokona inakujuza ile njia rahisi kuliko zote
Sawa kila mtu anaweza akawa anatumia PDF reader kufungua faili la PDF, lakini vipi kama huna PDF reader au programu hiyo ina matatizo kufungua faili la PDF?
Unaweza fungua faili la PDF kwa kutumia msaada wa kivinjari cha Google, GOOGLE CHROME. Kutokana na kuwa google chrome ina vipengele vingi kimoja wapo ni pamoja na kuwa na uwezo wa kufungua mafaili ya PDF. Hili linawezekana kwa sababu chrome yenyewe ina PDF reader ndani yake inayoitwa Chrome PDF Viewer ambayo inatumiaka kufungua faili lolote la PDF
Njia Za Kufungua Faili La PDF Kwa Kutumia Google Chrome
- Nenda sehemu ambapo kuna faili lako la PDF kisha ‘Right Click’
- Yatakuja machaguo mengi, utaona Open With click hapo na kisha chagua Google chrome
- Hivyo ndio namna unavyoweza ona faili lako la pdf au kwa ueahisi kabisa unaweza kuli ‘Drag’ (Kuckick bila kuachia na kusogeza na hatimaye kuachia) na kwenda kuliachia katika kivinjari cha google chrome
Kama Faili Lako La PDF Halifunguki Katika Google Chrome
Kama unapata matatizo katika kufungua faili la PDF kwa kutumia kivinjari cha chrome basi inabidi uitoe hiyo plugin ya Chrome PDF Viewer na uwezesha plugin ya Adobe Acrobat au Adobe Reader. Pia inawezekana kabisa kuwa hata hiyo Chrome PDF Viewer ikawa imesitishwa basi itakubidi uiwezeshe na kuangalia faili lako la PDF kama litafunguka. Kama Chrome PDF Viewer imewezeshwa sasa unaweza kuwezesha plugin za adobe reader pia
Njia Za Kuwezesha Plugin Ya Adobe Acrobat Au Adobe Reader
- Kwanza kabisa katika Google chrome sehemu ya kuandikia tovuti andika chrome://plugins au About://plugins
- Sasa tafuta Chrome PDF Viewer kisha click disable ili kuisitisha
- Kisha wezesha Adobe Acrobat au Adobe Reader plug-in kwa kuclick kwenye neno Enable
- Funga Eneo lako la Plugin na kisha anzisha tena Chrome yako na fuata maelekezo ya mwanzo kabisa ili kuweza kufungua mafaili ya PDF bila kutumia PDF reader.
No Comment! Be the first one.