Mara nyingi unaweza ukajikuta umejaza apps nyingi kwenye simu yako ya Android na ungependa kupunguza, tatizo linakuja ya kwamba una apps kibao na kazi ya kubofya moja moja itachukua muda wako mwingi.
Leo tunakuletea apps mbili bomba zaidi zinazoweza kukusaidia katika hili. Apps hizi zinafanikisha jambo hilo kwa kukuwezesha kuchagua apps zote unazotaka kuzitoa kwenye simu yako na kisha kubofya sehemu nazo zota zitatolewa, yaani ‘uninstalled’.
Apps mbili maarufu zinazoweza kukusaidia kufanya hivyo ni App Master (kwa jina jingine ni Unistall Master) na nyingine ni Easy Uninstaller.
Je zinafanyaje kazi?
- App zote hizi zitakupa orodha ya apps zote zilizopo kwenye simu au tableti yako na kukupa uwezo wa kuziondoa.
- Kingine spesheli kwenye App Master ni uwezo wa kurudisha app uliyoiondoa kimakosa. Yaani kama umebadilisha uamuzi basi unaweza ukarudisha app hiyo kupitia app hii.
- App Master inakupa uwezo hadi kuondoa baadhi ya apps zisizokuwa za ulazima zilizokuja na simu yako.
Je kwa nini ni muhimu uondoe baadhi ya apps mara kwa mara?
Kumbuka ya kwamba ni vizuri mara moja moja kukaa na kuondoa apps usizozitumia kwenye simu yako. Jambo hili linasaidia kuhakikisha simu yako inafanya kazi katika ufanisi mkubwa zaidi.
Kupakua apps hizi kutoka soko la Google Play;
Bofya -> App Master | Easy Uninstaller
App nyingine ambayo tushawahi izungumzia inayoweza fanya kazi hii ni ‘Clean Master‘, bofya hapa kuijua zaidi -> Clean Master: Moja App Muhimu Kuwa Nayo
No Comment! Be the first one.