fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Teknolojia

Ecocapsule: Kijumba Kiduchu cha Umbo la Yai Kwa Ajili ya Makazi ya Kisasa Zaidi

Ecocapsule: Kijumba Kiduchu cha Umbo la Yai Kwa Ajili ya Makazi ya Kisasa Zaidi

Spread the love

Wasanifu (Architects) kutoka nchini Slovakia (barani Ulaya) wamefanikiwa kutumia kiwango kikubwa cha teknolojia ya sasa katika ujenzi wa kijumba (unaweza kukiita ki-gheto) kidogo kinachokupatia makazi yaliyo kwenye kiwango cha juu popote utakapokuwa duniani. Ubunifu wa hali ya juu pamoja na utumiaji wa teknolojia ya kisasa unaonekana kuleta vitu vyenye kiwango cha juu kabisa.

Baadhi ya timu ya utengenezaji wa Ecocapsule wakiwa mbele ya kijumba kimoja

Baadhi ya timu ya utengenezaji wa Ecocapsule wakiwa mbele ya kijumba kimoja

Kwa zaidi ya muda wa miaka sita timu ya wasanifu hawa wanaojiita Nice Architects ilifanya kazi kuhakikisha utengenezaji wa vijumba hivi unatoka kutoka kuwa kwenye picha/michoro za kiubunifu hadi kuweza kuwa vijumba vya kweli vinavyoweza kutumika. Ni hivi karibuni tuu wasanifu hao waliweza kuonesha moja ya kijumba hicho katika maonesho ya kiubunifu kimataifa na sasa bidhaa yao ishaanza kuitajika kwa kasi.

Vijumba hivyo vimepewa jina la EcoCapsule

Mfumo wa umeme na maji

Mfumo wa umeme na maji

Sifa za Ecocapsule

  • Kina urefu wa takribani mita 8, na wenyewe wanasema watu wazima wawili wanaweza kuishi ndani yake.
  • Eneo la juu kuna teknolojia ya umeme wa nguvu jua (Solar), umeme huo pia unakuwa unachaji betri lilopo ndani ya kijumba hicho
  • Pia kuna upanga kwa ajili ya kufua umeme kutoka kwenye nguvu ya upepo
  • Inasemekana kwa vyanzo hivi viwili vya umeme unaweza kukaa eneo mbali na umeme ata kwa mwaka mzima na usikose huduma hiyo kabisa
  • Pia eneo lake la juu linaingiza maji ya mvua na kuyachuja na kuyaweka salama kwa ajili ya kutumika ata kwa kunywa. Maji yanahifadhiwa eneo la chini la kijumba hicho kwa ndani – yaani kuna kajitenki ka ndani kwa ndani
  • Wanasema ingawa unaweza kukaona kadogo kwa nje ila ndani yake utapata, chumba cha kulala chenye kitanda cha kinachoweza kukuchwa. Ukikunja kitanda unapata eneo zuri la kufanyia kazi zako.
  • Pia kuna choo, eneo la jiko pamoja na kajistoo kidogo. Stoo zipo mbili, kuna ka ndani na kengine unachoweza kukafungulia ukiwa nje.
  • Pia kajumba kamoja kanaweza kusafirishwa kwa urahisi kwa kuingizwa kwenye kontena moja au kwa kupakiwa katika katela kakuvutwa na gari za kawaida.
Wenyewe wanasema vijumba hivi vinafaa mahali popote pale

Wenyewe wanasema vijumba hivi vinafaa mahali popote pale

Hadi sasa wameshapata oda za manunuzi ya vijumba hivyo kwa maelfu, wenyewe wanasema hawakutegemea kama vingeitajika kwa namna hiyo. Bei bado haijawekwa wazi ila inaonekana haitakuwa ni bei rahisi sana. Vijumba hivyo vitaanza kuuzika ifikapo mwakani. Tayari hadi sasa wanasema kuna hadi mahoteli na watu mashuhuri wameanza kuwafuatilia kufahamu upatikanaji wa vijumba hivi.

[metaslider id=5014]

Watu wa mabara ya Ulaya na Amerika wengi wao wanapenda maisha ya kujaribu jaribu wakiwa mbali na makazi ya watu, yaani kama vile kwenye mapori n.k na inategemewa wengi wao ndio watavutiwa zaidi na vijumba hivi.

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania