fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps whatsapp

Brazil yaifungia WhatsApp tena!

Brazil yaifungia WhatsApp tena!

Spread the love

Jaji mmoja katika mahakama ya jimbo la Sergipe nchini Brazil ametoa hukumu ya kulazimisha mitandao ya simu ya nchini humo kuzuia huduma ya WhatsApp kwa muda wa masaa 72 kuanzia mchana wa tarehe 2 mwezi huu wa tano.

Jaji huyo anaitaka WhatsApp itoe data za mazungumzo yahusuyo wafanyabiashara wa madawa, data hizo zinatakiwa kupewa kwa polisi na huku WhatsApp wakisema hawana huwezo wa kutoa data hizo.

SOMA PIA  Kipya kwenye WhatsApp: Angalia picha/video mara moja tu!

Mitandao ya simu ya nchini humo ilibidi kuzuia huduma za WhatsApp kwani kutokufanya hivyo kungewaweka katika adhabu ya faini ya takribani dola $180,000 kwa siku (takribani Tsh 293,000,000 | Kes 18,000,000).

Mara ya mwisho huduma za WhatsApp kufungia nchini humo kulisababisha ukuaji mkubwa wa utumiaji wa app ya Telegram ambayo ni mpinzani mkubwa tu wa WhatsApp na inaonekana uhamuzi huu utazidi kukuza utumiaji wa Telegram.

Hii si mara ya kwanza, takribani miezi mitano iliyopita ilishafungiwa – Soma – Brazil: WhatsApp Ilipofungiwa Kwa Muda, Telegram Ilipata Zaidi ya Watumiaji Milioni 1.5 Wapya

Kutokana na mabadiliko ya kiusalama yaliyofanywa na WhatsApp kwa sasa ni vigumu sana ata kwa wao kujua mazungumzo yanayofanywa na watumiaji wao….hivyo dalili ya suala hili kufanikiwa ni dogo sana.

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania