fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps instagram Mtandao wa Kijamii

App ya Instagram kuja na muonekano mwingine

App ya Instagram kuja na muonekano mwingine

Spread the love

Muonekano mpya wa app ya Instagram ulio njiani kuanza kusambaa kwa watumiaji wa app hiyo waanza kupatikana kwa baadhi ya watumiaji wa app hiyo.

Kwa muda mrefu app ya Instagram haijafanyiwa mabadiliko yeyote makubwa ya kimuonekano tokea ujio wake na sasa inaonekana mabadiliko yanakuja.

Angalia picha zinazoonesha muonekana huo mpya uliombioni kupatikana kwa watu wote… Je unadhani kuna umuhimu wowote wa kubadilisha muonekano huo?

SOMA PIA  Twitter: Tweet ujumbe wa sauti, uwezo umeanza kwa iOS na unakuja kwa Android

Muonekano wa Instagram

Muonekano huu tayari umesukumwa kwenye updates za watu wachache huku wenyewe Instagram wakisoma maoni ya wale wanaopata app hiyo katika muonekano huu. Inasemekana kama utafurahiwa na watumiaji wengi basi muda si mrefu utapatikana kwa wote.

Ingawa ni muonekano mzuri ila kwa kiasi kikubwa unaleta mabadiliko makubwa sana ya kimuonekano kwa watu ambao wametumia app hiyo kwa kipindi kirefu.

SOMA PIA  Meseji Na Kupiga Simu Vyaja Ndani Ya Snapchat Ya Kompyuta, Lakini Ni Kwa Wateja Wa Snapchat Plus!

instagram kuja na muonekano

Unamaoni gani juu ya mabadiliko haya?

Picha na mtandao wa PhoneDog

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania