fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps

App 5 Bora Za Android Kwa Ajili Ya Kushusha (Download) Muziki!

App 5 Bora Za Android Kwa Ajili Ya Kushusha (Download) Muziki!

Spread the love

Muziki una sehemu kubwa sana katika maisha yetu. Mara nyingi tunasikiliza miziki tunayoipenda ili kujiridhisha na kupata faraja ya moyo.

Linapokuja swala zima la kusikiliza muziki unaweza ukasema simu zetu zimechukua majukumu mazima ya redio na hata vifaa spesho vya kucheza muziki maarufu kama vile iPod.

Karibia kila simu janja ina uwezo wa kuunganisha na intaneti au hata WiFi. Sasa kama simu yako inaweza ikaingia katika intanenti basi unaweza kabisa ukashusha nyimbo nyingi kadri kifaa chako kinavyoweza kupokea.

Tuachane na hayo, Ngoja tuzijue App Bora kwa ajili ya kushusha Muziki katika simu janja yako ya Android.

4shared Music

4Shared-Music app

4Shared-Music

– hii ni App spesheli ambayo imeandaliwa kwa wale ambao hawawezi kuishi bila ya muziki. Ndani ya App hii kuna kipengele cha ‘Tafuta’ (Search) ambapo mtu unaweza tafuta muziki unaoutaka na kuuweka katika ‘PlayList’ katika ‘4shared Music’. Pia unaweza ukatengeneza ‘PlayList’ yako mwenyewe na unaweza hata kupandisha miziki kutoka katika simu yako kwenda katika App hii. App hii inatoa GB 15 za bure ambazo mtumiaji anaweza akahifadhi miziki mingi katika App hii.

SOMA PIA  Huduma ya utumaji pesa ndani ya WhatsApp yaanza kupatikana

RockMyRun

RockMyRun

RockMyRun

– Hii app ni spesheli kwa wale ambao wanafanya mazoezi (hasa hasa asubuhi). App hii itakusaidia sana katika kufanya mazoezi kwa sababu inajulikana kama moja kati ya App nzuri zaidi za Mp3. Na pia App hii inafanya kazi na na ma’DJ wakali ambao wanatengeneza Mix kali kabisa ambazo zinaendana na mazoezi ya mwili.

SOMA PIA  Maelfu ya watumiaji wa app ya SnapChat hawajapendezwa na sasisho jipya

Kama wewe ni mtu wa Gym au mazoezi kwa sana inabidi kuwa na App hii

Anghami

Anghami

Anghami

– Hii ni moja kati ya app za Bure ambayo inahisha kushusha muziki katika simu zote za Android. Kwa kutumia App hii unaweza kushusha mamilioni ya nyimbo duniani katika kifaa chako cha Android.

Wynk

Wynk

Wynk

– Hii ni app ya kushusha miziki katika kifaa cha Android ambayo ina zaidi ya miziki milioni 1.8. Kwa haraka unaweza ukaishusha miziki hiyo au kuisikiliza bila kuishusha (Stream).

SOMA PIA  Tegemea Kuweza Kutumia Apps za Android kwenye Kompyuta

Sound Cloud

Muonekano Wa Sound Cloud muziki

Muonekano Wa Sound Cloud

–  Hii sio ngeni kwako sio? App hii ni nzuri na inatumiwa sana kwa wapenda muziki na hata wanamuziki wanaochipukia. Ina mamilioni ya watumiaji wenye furaha na huduma hii.Kwa kutumia App hii unaweza ukashusha muziki unaoutaka baada ya kuutafuta ndani ya App. Pia unaweza ukacheza muziki bila kuushusha (Stream) ndani ya App. Pia unaweza ukawafollow marafiki na kujua ni miziki gani wanasikiliza.

Sidhani kama kuna mtu ambaye hasikilizi muziki? (hata wachawi nadhani wanasikiliza). Niambie katika App hizo ni ipi ambayo unaipenda sana. Kwa habari kama hizi na za moto zaidi tembelea mtandao wako wa TeknoKona kila Siku. Kumbukua TeknoKona Daima Tupo  Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania