Wengi wetu na dunia nzima kwa ujumla inafahamu kuwa tayari Android 11 imeshatoka na simu janja mbalimbali zimeshaanza kufahamika ni lini zitapata taarifa fupi ya kuweza kupakua toleo jipya la programu endeshi na pengine watumiaji wa rununu (Nokia) walikuwa wanajiuliza pia.
Miaka ya 90 hadi 2000 simu za Nokia zilikuwa maarufu sana duniani lakini baadae zikapotea halafu mambo yakageuka na kwa miaka ya karibuni tumeweza kushuhudia rununu nyingi tuu sokoni ikiwemo muundo mpya wa Nokia 3310. Si suala la kubisha kuwa hivi sasa HMD Global wamejitahidi vilivyo kurudisha heshima ya Nokia ingawa ushindani nao umeshika hatamu!.
Sasa kuna suala la simu janja za Nokia kuweza kupakua toleo la Android 11 na kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka HMD Global wameeleza ni lini rununu mbalimbali (Nokia) zitaweza kupokea taarifa kuhusu kuweza kuhamia kwenye toleo la programu endeshi tajwa:
-
Kwa kuanza Nokia 2.2, 5.3, 8.1 na 8.3 5G ndio zitakuwa za kwanza kuweza kupata kupakua Android 11 ambapo kwenye robo ya nne (kati ya Mwezi Oktoba-Desemba) au mwezi Januari-Machi 2021 ndio suala hilo litawezekana.
-
Machi 2021, Nokia 1.3, 2.3, 2.4, 3.4 na 4.2 zimepangwa kwenye ratiba ya kuweza kuhamia Android 11 halafu kwenye nusu ya mwaka mwakani Nokia 3.2, 6.2 na 7.2 zitapata pia.
-
Kwenye robo ya pili (mwezi Machi-Juni) mwaka 2021, Nokia 1 Plus na Nokia 9 PureView zitapokea toleo hilo jipya la programu endeshi kutoka familia ya Android.
Hizo ndio simu janja za Nokia zilizo kwenye mlolongo wa kupokea taarifa fupi ya kuweza kuhamia toleo la jipya la programu endeshi swali ni je, rununu (Nokia) unayotumia ipo kwenye orodha?
Vyanzo: GSMArena, XDADevelopers
4 Comments