Fikiria, kosa moja tuu la uandikaji ‘code’ katika kompyuta lisababishe upoteze biashara yako kubwa ya miaka mingi!!!! – Hilo ndilo lilimtokea kijana Marco Marsala wa huko barani Ulaya.
Kwa bahati mbaya aliiambia kompyuta yake ifute kila kitu kwenye ‘servers’ zake ambazo anatumia kutoa huduma za Hosting kwa wateja zaidi ya 1535.
Kutokana na kosa hilo alisababisha ufutwaji wa data zote za mitandao mbalimbali ya wateja wake, na ubaya zaidi ata ‘Backups’ zake zilizokuwa kwenye hard disk zenye ujazo mkubwa zaidi zilikuwa zimeunganishwa na servers hizo kwa wakati huo – hivyo nazo zikafutwa pia.
Ubaya njia aliyotumia sio ya kufuta na kisha kufuata kitu kwenye ‘Recycle bin’, njia aliyotumia inahusisha utumiaji wa code inayofuta vitu kabisa kabisa tena bila ata ya kukutaarifa kukuomba uhakika wa kile unachokifuta. Code hiyo ni “rm -rf”.
Maana ya code ya ‘rm -rf’, rm inaiambia kompyuta itoe (remove) mafaili husika, r inayofuatia ndiyo inaiambia ifute kabisa (delete) na f inamaana ya ‘force’, yaani kwa ulazima huu ina maanisha kompyuta isiulize maswali yeyote na ifute mafaili husika.
Bwana Marco Marsala alioomba msaada kwa mabingwa wa mapo ya servers, wapatikanao katika forum ya mtandaoni ifahamikayo kwa jina la ‘Server Fault’.
Na wengi walimwambia ni vigumu tena yeye kuweza kupata data hizo alizofuta. Na ata kama atatumia makampuni makubwa ya masuala ya ‘kurecover’ data zilizofutwa basi itamgharimu kiasi kikubwa sana cha pesa na ni kazi inayoweza chukua muda mrefu sana (miezi na miezi) kutokana na ukubwa wa data alizozifuta. Kwa kifupi wengi walimwambia alie tuu na ajiandae kwa kesi zitakazofunguliwa dhidi yake na wateja wake.
Ushawahi kuformat diski yako yenye data muhimu kwa bahati mbaya? Nadhani utakuwa unafahamu machungu yake, sasa huyu amepoteza bishara yake ya miaka mingi kwa kosa hilo hilo…Majangaaa…
Chanzo: IndiaTimes.com na Independent.co.uk