Baada ya upatikanaji wa huduma ya WhatsApp kwenye kompyuta kupitia kivinjari cha kompyuta kama vile Chrome na Firefox sasa WhatsApp wameamua kuleta programu spesheli kwenye kompyuta – Windows na Mac.
Ujio huu unaweza ukawa mwanzo wa uletaji pia wa uwezo mbalimbali kwa toleo la WhatsApp la kompyuta. Muda si mrefu tusishangae pale tutakapoona WhatsApp ikizidi kujitutumua katika kutumiwa kwenye kompyuta kushindana na programu ya muda mrefu ya mawasiliano kwenye kompyuta ya Skype.
Kwa sasa kama unataka kupakua programu hii kwenye kompyuta yako tembelea -> https://www.whatsapp.com/download
Soma pia makala za maujanja na habari za WhatsApp -> TeknoKona/WhatsApp