fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Sayansi

NASA: Uharibifu wa mazingira kubadilisha mzunguko wa Dunia

NASA: Uharibifu wa mazingira kubadilisha mzunguko wa Dunia

Spread the love

Imebainika kwamba uharibifu unaofanywa katika mazingira yetu unaenda kuathiri namna ambayo dunia inazunguka, hii ni kwa sababu mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokana na uharibifu wa mazingira unasababisha kuyeyuka kwa theluji iliyokuwa imeganda katika pembe za dunia hivyo kubadilisha kuhamisha uzito wa dunia kutoka katika pembe za dunia.

Tangu tukiwa watoto shuleni  tulifundishwa kwamba dunia hulizunguka jua kutengeneza majira ya mwaka na wakati huo huo dunia huwa inazungua katika muhimili wake kutokea magharibi kwenda mashariki mzunguko huu ndiyo unahusika na kuwepo kwa mchana na usiku.

SOMA PIA  Hoteli ya kwanza ya juu ya Anga kufunguliwa mwaka 2022

Mazingira

Kitu ambacho wengi wetu tulikuwa hatujui ni kwamba mzunguko wa dunia katika muhimili wake kunachangiwa na mgawanyo wa uzito wa dunia yenyewe pamoja na mambo mengine yote, ili kuielewa hii dhana basi tuchukue mfano wa mpira wa kikapu kisha uuzungushe juu ya kidole kimoja mpira huu huzunguka na kukupa nafasi ya kubadili hata kidole kinaushikilia hii yote ni kwasababu uzito wa mpira unagawanywa sawasawa pande zote.

Kwa dunia lakini hali nitofauti na mpira wa kikapu, dunia uzito wake mwingi umejikita katika pande za dunia. Lakini kutokana na uharibifu wa mazingira theluji ambazo zipo katika pande za dunia zimekuwa zikiyeyuka kwa kasi na hivyo kusababisha dunia kuanza kupoteza mwelekeo wa mzunguko wake.

Kwa mujibu wa Watafiti wa NASA kutoka katika maabara zao wanasema kwamba dunia imeanza kuondoka katika mzunguko wake wa asili, na watafiti hao wamesema kwamba hii inatokana na uharibifu wa mazingira kusababisha theluji katika pande za dunia kuyeyuka na kusababisha mgawanyo wa uzito kubadilika.

SOMA PIA  Schiaparelli: Chombo maalum cha anga kutua katika sayari ya nne

Watafiti hao mwishoni wametoa wito kwa binadamu kufanya jitihada za kutosha na za makusudi kuzuia uharibifu wa mazingira ili tuweze kutunza dunia ili tuweze kuishi maisha marefu na pia wajukuu zetu waweze kuishi na kuwaachia wajukuu wao.

Chanzo: Engadget pamoja na mitandao mingine

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania