Jana katika hoteli ya Hyatt Regency, maarufu kama Kilimanjaro kulifanyika uzinduzi wa huduma za intaneti za kiwango cha 4G kutoka kampuni mpya ya Smile Tanzania.
Smile Tanzania wamekuwa kampuni ya kwanza kuleta huduma ya kiwango hicho Tanzania, na pia kuifanya Tanzania kuwa moja ya nchi chache Africa na duniani kwa ujumla kupata huduma ya 4G.
Ni nini tofauti kati ya 3G na 4G?
3G intaneti inauwezo wa spidi ya 600Kb hadi 1.4Mb kwa sekunde, na ikiwa ya juu kabisa basi inauwezo wa kufikia Mb 3.1 kwa sekunde, lakini kupitia 4G uwezo wa spidiumeongezeka hadi kufikia kati ya Mb 3 hadi 6 kwa sekunde, na kukiwa na hali nzuri basi inaweza fikia hadi Mb 10 kwa sekunde! Hivyo kwa mwendo kasi huo unauwezo wa kushusha (download) faili kubwa la GB kadhaa ndani ya dakika chache tuu.
Je vipi kuhusu gharama?
Kwa kifupi gharama ipo juu ukilinganisha na gharama za mitandao ya simu mingi. Kupitia mtandao wao, gharama ya GB moja kwa mwezi inapatikana kwa Tsh 16,000 wakati GB 3 ni Tsh 36,000/=. http://www.smile.co.tz/~smiletz/pages/services/data-bundles.php
Inapatikana wapi?
Kwa sasa huduma za Smile bado ni kwa jijini Dar es Salaam tuu, itabidi tuwape muda kidogo. Ni matarajio yangu hawatabakia hapa hapa.
Nategemea kuja huku kwa 4G kupitia Smile kunaweza kukaleta chachu kwa mitandao mingine mikongwe ya simu kufanya hivyo pia.
No Comment! Be the first one.