Nyayo zinazoaminika kuwa ni za binadamu wa kale zimegunduliwa katika kisiwa cha Crete barani Ulaya, uvumbuzi huu huenda ukabadili historia ya binadamu wa kale.

Habari hii imepokewa kwa mitazamo tofauti tofauti kwa makundi tofauti kwa kuwa Kwa miaka mingi imekuwa ikiaminika binadamu wa kale kabisa waliishi Afrika hasa maeneo ya Afrika mashariki.
Nyayo hizi mpya zimegundulika katika kisiwa kidogo cha Trachilos huko Crete, zipo jumla ya nyayo 29 ambazo zina ukubwa tofauti tofauti kuanzia milimita 94 hadi milimita 223. Nyayo hizi zinaosadikiwa kuwa zimekuwako ardhini kwa miaka milioni 5.7 ni ushahidi tosha kwamba kile kilichokuwa kinajulikana miaka na miaka huenda kisiwe cha ukweli.

Tayari mijadala imeibuka hasa juu ya uhalali wa ushahidi huu, lakini wanasayansi hao wamesisitiza juu ya uhalali wa njia waliyotumia kujiridhisha kwamba nyayo hizo zilizoachwa ni nyayo za binadamu wa kale.
Ingawa wapo wanaobeza chapisho hili lakini wanasayansi hawa wawili kwa pamoja wamekwisha chapisha machapisho ya kisayansi karibu 600 ambayo yanahusiana na nyanyo za binadamu wa kale. Hii inamaana kwamba sio tu wanaelewa wanacho kisema bali kuna uwezekano mkubwa wakawa sahihi kwa asilimia 100.
Uvumbuzi huu huenda ukabadilisha historia ambayo imekuwa ikifahamika kwa miaka mingi, mahali ambapo binadamu wa kale aliishi. Hata hivyo bado kazi kubwa inatakiwa kufanywa juu ya tafiti zaidi ili kupata taarifa zaidi juu ya nyayo hizo, na pengine walau utafiti kuona kama kuna mabaki mengine yanaweza kupatikana ili yaweze kutoa taarifa zaidi.
Uvumbuzi huu hata hivyo umekuja miezi michache baada ya uvumbuzi mwingine ambapo kuligunduliwa masalia yenye umri wa miaka milioni saba ya jino la mnyama ambaye anafanana na nyani, masalia ya mnyama huyu ambaye amepewa jina la “El Graeco” ndiyo masalia yenye umri mkubwa zaidi.
Hii inapelekea baadhi ya wanazuoni kufikiri kwamba pengine binadamu wa kale aliishi Ulaya.
Jisomee chapisho kuhusu uvumbuzi huu hapa