Muda mwingine mwanga wa laptop unaweza ukawa mdogo sana na wakati mwingine unakuwa mkubwa sana. Je unafahamu njia gani za kupunguza mwanga wa laptop yako? Leo tutakupa kadhaa, tuna uhakika mojawapo ni unayoifahamu kwa sana na zingine mbili inawezekana ikawa ni mara yako ya kwanza kuzifahamu.
Njia ya Kwanza: Tumia Kibodi (Keyboard)
Hii ni njia maarufu zaidi iliyozoeleka kwa wengi, ila tuu kama laptop yako inakuja na uwezo huo katika keyboard yake.
Utumiaji wa ‘Fn’, kwenye laptop nyingi za kisasa ukishikilia kwa kidole kimoja eneo la Fn kisha ukibofya kwenye kibodieneo la alama za mshale wa kushoto na kulia utaweza kupunguza na kuongeza mwanga wa laptop. Njia nyingine pia huwa inahusisha kushikilia ‘Fn’ na kisha kubofya F7 kwa ajili ya kupunguza mwanga na kushikilia Fn kisha kubofya F8 kwa kuongeza mwanga.
Njia ya Pili; Tumia programu spesho, leo tutakuletea programu mbili kwa watumiaji wa laptop za Windows.
Volumouse; Haka ni kaprogramu kadogo chenye ukubwa wa takribani kb 100 tuu.
Kwa programu hii utaweza kupunguza na kuongeza mwanga wa kompyuta yako kwa kutumia kipanya (mouse) ya laptop yako, yaani kwa kutumia eneo la gurudumu kwenye kipanya ambalo mara nyingi huwa linatumika kwa ajili ya kushusha kurasa juu au chini utaweza kuongeza na kupunguza mwanga wa laptop yako. Ukishapakua programu hii basi hakikisha unaenda kwenye mipangalio (settings) zake na kuchagua hapa kwenye picha chini, yaani ukishikilia kwa kidole kimoja eneo la ‘Ctrl’ bila kuachia na kisha kuzungusha kigurudumu cha kwenye kipanya chako basi utaweza kupunguza na kuongeza mwanga wa laptop husika.
Unaweza kulishusha faili la Volumouse hapa | Bofya
DimScreen; Hii programu nyingine nyepesi kwa ajili ya watumiaji wa kompyuta za Windows. Faili lake lina ukubwa wa kb 400 tuu.
Ukishapakua programu hii basi itakuwa inajionesha katika lile kundi la programu zinazofanya kazi zinazowekwa kwenye eneo la karibu na alama za spika na muda, kwenye kona kulia (Tray) ; angalia picha. Ukifika hapo bofya programu hii kwa kutumia upande wa kulia wa kipanya (mouse) chako na utaona uchaguzi wa kiwango cha mwanga cha kuanzia asilimia 0..10.. hadi 90. Pia kama hii haitoshi utaweza pia kuchagua namna nyingine ya kuweza kuwa unaongeza na kupunguza mwanga kwa kutumia eneo la kibodi unalolitaka.
Unaweza kilishusha faili la DimScreen hapa | Bofya
No Comment! Be the first one.