Bobby Kotick amekua na kampuni ya Activision Blizzard kwa muda na sasa na mpaka kufikia disemba 29 atakua ameshakamilisha mambo yote kuhusiana na kampuni hiyo.
Kingine ni kwamba sio yeye tuu katika kampuni ya Activision Blizzard ambae anaagana na kampuni hiyo bali kuna wafanyakazi wengine nao wanaondoka katika kampuni.
Mabadiliko haya yanatokea muda mchache baada ya kampuni ya Microsoft kukamlisha ununuzi wa kampuni hii nguli ya magemu duniani.
Kumbuka ununuzi huu ndio unakua mkubwa sana katika historia ya magemu maana ndio ambao unahusisha pesa nyingi sana.
Dili hili pia lilisababisha pia mpaka mamlaka kuingilia kati na kufanya uchunguzi ambao nao umetumia muda mrefu mpaka kuja kupewa kibali cha kuendelea na mauziano hayo
Ni wazi kabisa inaonekana kwamba kampuni ya Microsoft inataka kuweka uongozi ambao unaujua vizuri ambao kampuni inahisi itaendana nao vizuri tuu.
Bwana Bobby yeye ameweka wazi kupitia katika mitandao ya kijamii kwamba ameamua kuachana na wadhifa huo katika kampuni hiyo.
Lakini kingine kikumbukwe ni miezi miwili tuu imepita tangia Xbox nao wabadilishe viongozi wa juu katika kampuni hiyo.
Pengine kwa haraka haraka itakua ni kuna hali ambayo Microsoft inataka kitengo/kampuni yake ya magemu iwe japo bado wanafanya vizuri tuu katika soko.
Mara kwa mara makampuni yakinunuliwa huwa uongozi unabadilishwa ni mara chache viongozi huwa wanabakizwa wale wale tuu.
Ningenependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je udhani kwa mabadiliko haya kuna kitu kimejificha? Au ni moja ya njia ya kusonga mbele?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.