Kwa sasa simu za Microsoft maarufu kama Windows hazipo katika mstari wa mbele katika kampuni hilo. Sio jambo lililojificha kwa kila mtu anajua kama haizifanyi vizuri kama kampuni hilo linavyotaka.
Simu hizi toka Microsoft hazina wapenzi wengi kiasi cha kwamba kuna watu amabao hawataki hata kuzisikia kabisa – je wewe ni mmoja wao? – ukiachana na hilo sio kwamba kampuni itaachana na biashara ya simu hizo bali itakuwa haipewi kipaumbele kama mwanzoni.
Windows katika simu janja inashika namba tatu kama Os yenye uwezo mkuwa nyuma ya iOS ya Apple na Android ya google.
Vifaa ambavyo kampuni inavinagalia kwa macho matatu ni pamoja na Microsoft Surface na huduma zake za michezo (gemu) maarufu kama Xbox.
Kwa mwaka 2016 kampuni limeona ni bora kuendelea kidedea kwa vitu ambavyo vilikubalika vikubwa kwa wateja wao.
Simu nyingi kutoka Microsoft zinajulikana kwa kuwa na vioo/skrini kubwa kwa mfano Lumia 950 ina kioo cha inchi 4. Kama Microsoft wana mpangi wa kuwa na simu ndogo alafu zenye uwezo mkubwa — kama iphone walivyofanya katika iPhone SE – wanaweza wakawateka wateja wengi sana.
Inaweza ikaingia akilini kwamba simu ndogo zenye uwezo mkubwa zinaweza zikaleta faida kubwa kwa kampuni.
Inaonekana kuwa kampuni linawaachiwa wale ambao wameliteka soko la simu janja (Apple na Google)wabaki kutesa katika soko la simu kwa muda. Kampuni inachofanya ni kuwekeza nguvu zake nyingi katika eneo wanalolitawala.