Kwnye dunia ya leo makampuni mengi ambayo yapo kwenye ushindani yanapambana kuweza kuja na bidhaa ambazo zitavutia wateja wengi. Hivi nikuulize unajisikiaje ukiwa na chaji ambayo inajaza betri ndani ya robo saa tu?
Oppo ni moja ya kampuni ambayo inatoa simu janja za kuvutia lakini pia zenye sifa zilizoshiba. Mbali na hilo wamekuwa wakiweka nguvu ya kutengeneza kimemeshi (chaji) ambayo ina teknolojia ya hali ya juu ikiwa na uwezo wa kuchaji simu janja ndani ya muda mfupi.
Oppo wanazidi kwenda mbele kwenye tenolojia ya kuchaji simu janja ndani ya muda mfupi ambapo hivi sasa wametoa chaji yenye uwezo wa kujaza umeme ndani ya robo saa tu! Kimemeshi hiki kina 150W na kwa majaribio yaliyofanyika kwenye betri lenye 4500mAh lilijaa chaji ndani ya dakika 15 tu.
Katika majaribio ya kupima uwezo wa kimemeshi simu janja yenye betri lenye 4500mAh iliwashwa na kuanza kuchajiwa na ilichukua dakika 5 tu kutoka 0% hadi 50% na ndani ya robo saa (dakika 15) ilikuwa imeshafika 100% lakini wakati wote huo ilikuwa katika mfumo ambao rununu haiwezi kupatikana hewani (Airplane mode).
Uwezo wa chaji ya 150W kulinganisha na 60W ambazo zote ni za Oppo. Hii ya 60W inachukua karibu dakika 40 kujaza betri mpaka 100% kulinganisha na dakika 15 kwa kutumia kimemesheshi chenye 150W.
Uhai wa betri
Ni wazi kuwa kila chenye mwanzo kina mwisho wake na hizi simu janja zina kipengele cha “Afya ya betri” ambapo kama simu haijatumika (mpya) afya ya betri inakuwa ni 100% na itakuwa inapungua kadri ambavyo itakuwa inachahiwa. Sasa kwa kutumia hii SuperVOOC 150W itatumika mara 1600 ya kuchaji simu janja afya ya beti kushuka kutoka 100% hadi 80%.
Hizi chaji nyingine zenye trknolojia ya kuchaji haraka inachukua mizunguko 800 kushusha ayfya ya betri kutoka 100% hadi 80%.
Oppo wameweka wazi kuwa tayari wanatengenza kimemeshi cha 200W lakini pia ipo chaji iliyo katika hatua za majaribio ya ndani kwa ndani ya 240W yenye uwezo wa kuchaji betri la 4500mAh ndani ya dakika 9 tu!
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
No Comment! Be the first one.