App ya WordPad ni ya muda mrefu sana na ilikua inakuja moja kwa moja katika kompyuta zenye programu endeshi ya windows.
Kwa kipindi cha zaidi ya miaka 29 programu hii ya wordpad imekua ikipatikana ndani ya programu endeshi ya windows kutoka microsoft katika kompyuta zote.
Kwa sasa Microsoft imeseama inaachana kabisa na programu hiyo kwani kwa sasa kompyuta zitakua zinakuja na App ya Notepad.
Cha kushangaza ni kwamba bado hakuna uwazi wa asilimia 100 kwa Notepad ndio mrithi wa moja kwa moja wa WordPad.
Kumbuka WordPad ina vipengele vyote ambavyo vinapatikana katika programu ya Microsoft Word hivyo basi ukiwa na Notepad bado utakua na uwezo wa kuaandaa machapisho bila hata kuwa na MS Word.
Kingine ni kwamba App ya WordPad haitakua na uwezo wa kupatikana tena maana sasisho (uupdate) lijalo la Windows 11 litakuja bila App hiyo.
App hii imeanza kutumika kwa mara ya kwanza kabisa katika Windows 95 na hii imekua kwa matoleo mengi kwa miaka mingi lakini mwisho wake ni toleo la windows 11.
Kingine ni kwamba kwa dunia ya leo ni ngumu sana kumuona mtu anatumia App ya WordPad kama njia yake kuu ya kufanya machapisho.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je ushawahi kutumia App ya WordPad? Je ni sawa kwa kampuni kuachana nayo kabisa na kuanza kutumia App zingine ambazo zinafanana?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.