fbpx
Kompyuta, Microsoft

Mwalimu wa ICT anayefundisha Microsoft Word bila Kompyuta!

mwalimu-wa-ict-anayefundisha-microsoft-word-bila-kompyuta

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Mwalimu mmoja wa somo la ICT (Information and Communication Technology) nchini Ghana ametambuliwa katika ulimwengu kwa madhira anayopata katika ufundishaji wa somo hilo la mambo ya elimu ya kompyuta kwa wanafunzi wake.

Kwa kawaida somo hilo hufundishwa kwa nadharia na vitendo ambapo vitendo ni lazima kuwepo na Kompyuta ili wanafunzi waelewe kinachofundishwa. Mwalimu Richard Appiah Akoto anafundisha programu ya Microsoft Word kwa kulazimika kuchora ubaoni na kutumia chaki za rangi tofauti ili somo lake lipate kueleweka kwa wanafunzi.

INAYOHUSIANA  Microsoft Waleta Nokia 215 kwa Buku 50 tuu!
Mwalimu Akoto akiwa katika mkutano wa Microsoft kuhusu utoaji wa elimu.

Shule hiyo iliyo na miaka 14 tangu kuanzishwa kwake haijawahi kuwa na kompyuta ya aina yoyote shuleni hapo. Wanafunzi wake wanatarajia kufanya mtihani wa taifa na moja ya mtihani utakaowafanya kufaulu kwenda elimu ya sekondari ni wa ICT ambapo kama watafeli hawataruhusiwa kujiunga na sekondari.

Mwalimu Akoto alituma picha zake mwenyewe katika akaunti yake ya Facebook akionesha anavyojaribu kuelezea Kompyuta licha ya kutokuwa na Kompyuta halisi. Akoto anasema sio mara ya kwanza kufundisha Microsoft Word kwa kuchora ubaoni, amekuwa akifanya hivyo tangu alivyoanza kufundisha shuleni hapo.

INAYOHUSIANA  Google Waondoa Uwezo wa Watu Kufanya Mabadiliko Ktk Google Maps
Mwalimu Akoto akichora muonekano wa ukurasa wa Microsoft Word ubaoni.

Akoto ana kompyuta yake binafsi lakini haitumii kufundisha katika darasa kwa sababu anahitaji kuwa na kompyutaza mezani (Desktop) ambapo atawaelekeza namna ya kuunganisha kifaa kimoja baada ya kingine mfano Mouse, Keyboard, Monitor, n.k kama mtaala wasomo husika unavyoeleza.

Msaada wa kompyuta pamoja na vitabu vya komyuta kwa shule anayofundisha mwalimu Akoto.

Kwa ulimwengu wa sasa somo la ICT ni muhimu kufundishwa mashuleni lakini changamoto kubwa kwa shule nyingi barani Afrika ni kutokuwa na kompyuta za kufundishia wanafunzi.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.