fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Mtandao

Kumbuka Jina La ‘Movie’ Kwa Kutumia Mtandao Huu!

Kumbuka Jina La ‘Movie’ Kwa Kutumia Mtandao Huu!

Spread the love

Hivi ni mara ngapi umejaribu au umekuwa ukimuhadisia mtu kuhusu ‘Movie’ Fulani lakini ukawa hukumbuki jina lake? Kwa kutumia mtandao huu hilo halitakuwa ni tatizo tena

Mda mwingine unaweza ukamuhadisia mtu ‘movie’ Fulani uliyoiona lakini ukajishangaa tuu hukumbuki vizuri jina lake na ukajikuta unatoa jina la ‘movie’ nyingine kabisa.

Kwa kutumia mtandao wa whatismymovie.com hilo halitakuwa tatizo kabisa. Mtandao huu utakusaidia kujua jina la ‘Movie’ yako

Jinsi ya kutumia mtandao huu ni rahisi sana kwani itakubidi uandike baadhi ya maneno au uelezee kidogo jinsi movie hiyo ilivyo au nani ameigiza na ameigiza vipi. Maneno haya ni vizuri yakawa katika sentensi moja tuu.

SOMA PIA  Facebook Imekuja Na Mpangilio Mpya Wa Makundi (Group)!

Katika mtandao huo ukiufungua utakuatana na sehemu ya kutafuta (search) amabapo itakubidi kuandika maelezo yako kuhusiana na ‘Movie’ hiyo. Maelezo hayo yanaweza yakawa yanaelezea waigizaji, waandaaji, aina ya ‘Movie’ na kuendelea. Kwa mfano unaweza ukaandika

Baada Ya Kutafuta ''two girls tie a man at a chair pretending to be under 18'' Limepatikana Jina Sahihi La Sinema Ambalo Ni 'Knock Knock'

Baada Ya Kutafuta ”two girls tie a man at a chair pretending to be under 18” Limepatikana Jina Sahihi La Sinema Ambalo Ni ‘Knock Knock’

 itakuletea ‘Movie’ ya Keanu Reeves, Knock Knock

SOMA PIA  TTCL Kukodisha Muunganisho wa Intaneti Kwa Uganda

Baada ya ku ‘click’ tafuta (search) itatokea list kubwa tuu ikihusisha majibu ambayo yanahusiana na ulichokiandika (kukitafuta). Ukitaka kupata majibu sahihi kabisa  mtafutaji anaweza aka’click’ eneo ambalo limeandikwa “Good Match”  kama alichokitafuta amekipata au aneweza aka’click’ kwenye “Bad Match” kama alichokitafuta hakijatokea kama alivyokuwa akitarajia

Majibu yako yatahusisha jina la ‘Movie’ hiyo pamoja na mwaka ilipoachiwa, kava lake na maelezo mafupi juu yake.

Matandao wa whatismymovie.com umeanzishwa na kampuni ya Valossa. Pia mtandao huu hauna kazi ya kukuambia jina la ‘movie’ tuu bali pia inaweza ikakuambia ‘movie’ gani ya kuangalia kwa mfano unaweza ukaandika “Find all Avengers Movies” na mtandao utaleta zote za Avengers hii itakusaidia kama kuna zile ulizoziruka katika mtiririko huo kuweza kuzitafuta na kuziangalia.

SOMA PIA  Nintendo Kuitema Facebook na Twitter!

Hayo ndio maajabu ya Teknoloojia, karibia kila siku kinawezekana siku hizi, bado inazidi kukuwa kwa kasi. Kwa kutumia njia hii unaweza ukapata msaada wa nguvu tuu kuhusiana na ‘Movie’.

Kwa wale wapenda ‘Movie’ leo najua nimewaguswa.Niandikie sehemu ya Comment hapo chini juu ya jinsi ulivyoguswa.  Ili kuendelea kuguswa zaidi tembelea mtandao wako pendwa wa Teknokona kila siku. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania