fbpx

Jiwe Florence kupita karibu na sayari Dunia. #Sayansi

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Mawe kadha wa kadha yameshawahi kupita karibu na uso wa dunia lakini jiwe Florence ni kubwa kuliko yote yaliyowahi kupita karibu na sayari yetu.

Kitendo cha jiwe hili kupita karibu na dunia kinatokea karibu karne moja iliyopita na linatarajiwa kupita umbali wa takribani milioni 7. Jiwe la Florence linakadiriwa kuwa na kipenyo (diameter) cha kilometa 4.4.

Wanasayansi wa anga wanasema ingawa ni kubwa sana na ambalo linaweza kuleta madhara makubwa kama likigongana na sayari, watu waondoe hofu. Jiwe hilo halina hatari yoyote kwetu kwa sasa, LABDA karne nyingi sana huko mbeleni. 🙂

ANGA JIWE FLORENCE

ANGA JIWE FLORENCE

Jiwe la Florence – lililogundulika mnamo mwaka 1981; linaweza kuwa mara 18 ya wastani wa umbali kati ya Dunia na Mwezi. Ni jiwe kubwa kubwa zaidi kuwahi kupita karibu na dunia yetu tangu kuanzishwa kwa mpango wa shirika la anga za mbali la Marekani NASA, katika mpango wa kuchunguza na kubaini mawe yaliyopo karibu na sayari Dunia.

Kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2017 Florence ni jiwe la angani lililopo kwa kukadiria tangu mwaka 1890 na ukaribu huo hautawahi kutokea hadi baada miaka 2500.

Jiwe hilo ni rahisi kuliona kwa kutumia kifaa cha uchunguzi si kwa sababu tu ni kubwa lakini pia kwa sababu huakisi 20% ya mwanga wa Jua ambao huchoma kwenye sehemu yake ya chini na kinyume chake Mwezi huakisi 12% pekee.

Kitu chenye ukubwa wa  jiwe Florence kinaweza kuleta athari kubwa kama kikigonga Dunia. Wanasayansi wanaamini kuwa sasa wamebaini zaidi ya 90% ya miamba ya aina hiyo ya kutisha inayopita angani karibu na sayari yetu.

Chanzo: BBC

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.