Udukuzi kwenye Instagram. Kama kuna kitu knachokera na kusumbua watu wengi katika ulimwengu wa teknolojia udukuzi ni tatizo kubwa ambalo bado halijapatiwa ufumbuzi.
Kutokana na hali halisi jambo la kutotumia mitandao ya kijamii kwa jinsi teknolojia inavyokwenda hivi sasa si jambo rahisi kwa yeyote yule ambaye anaweza akatumia mitandao ya kijamii kuweza kufikia wengi duniani kuacha kutumia mitandao ya kijamii.
Instagram imegundua dosari katika mfumo wake iliyofichua nambari za simu za watu maarufu pamoja na anwani zao kwa wadukuzi wa mitandao.
Kilichofanyika katika udukuzi huo.
Instagram imesema kuwa nywila hazikuibiwa lakini ikawaonya wateja wake kuchunguza mienendo isiokuwa ya kawaida katika akaunti zao ingawa haikuweka wazi akaunti za watu maarufu zilizoathiriwa kutokana na udukuzi huo. Dosari hiyo ya kiusalama wa mitandao ilitokea kutokana na tatizo katika programu ya kampuni hiyo.
Instagram ambayo inamilikwa na Facebook baada ya kununuliwa mwaka 2012 kwa $1bn tayari umewasiliana na watu ambao akaunti zao zilidukuliwa ili kuwaelezea dosari iliyotokea. Instagram ina zaidi ya wateja milioni 700 duniani huku wateja milioni 300 wanautumia mtandao huo mara moja kwa siku.
Ingawa udukuzi huo umesharekebishwa lakini Instagram imewaonya wateja wake kuwa waangalifu kuhusu simu wasizotarajia, ujumbe na barua pepe.
Vyanzo: Fox News, BBC