Njia hii itazuia marafiki kuweza kujua kama umesoma meseji zao. Kumbuka kwenye WhatsApp kama ukiweka akaunti yako kutoweza kutumia tiki za bluu basi hiyo ni kwa meseji unazotuma na zile unazotumiwa zote hazitakuwa na tiki ya bluu.
Kuna njia rahisi ya kusoma meseji bila kuzima uwepo wa tiki ya bluu. Usomaji huo kwa upande mwingine hautatoa tiki ya blu katika ujumbe utakaosoma.
Ulishawahi mkwepa mtu katika mtandao wa WhatsApp lakini ungependa kusoma alichotuma? japokuwa tiki hizo za blu zinafanya zoezi lionekane gumu lakini kuna njia rahisi kabisa za kukabiliana nalo
NJIA
- pindi utakapopokea meseji usiifungue na unaweza kufunga ‘Notification’ yoyote itakayojitokeza.
- Fungua ‘Airplae Mode’ ambayo itazuia matumizi ya WiFi, Data na Kuzuia Meseji nyingine kuingia
- Hapo sasa, fungua WhatsApp kusoma meseji yako kikamilifu
- Funga WhatsApp kabisa na kisha toa Airplane mode. Licha ya kuwa umeisoma meseji hiyo lakini tiki za blu hazitatokea.
Hongera umeweza kusoma meseji bila mtu aliyekutumia kujua kama umeisoma. Njia hii ni nzuri sana kwani itakusaidia kusoma ujumbe kwa mtu ambae kwa upande mwingine ulikuwa huna haja ya kumjibu kabisa.
Usipowajibu watu wanajisikia vibaya sio, tena haswa pale wanapokuwa na ushahidi kuwa umesoma meseji zao. Kama njia hii unaiona ngumu unaweza kubofya Hapa ili kuona njia nyingine
No Comment! Be the first one.