WhatsApp ndio App inayotumika sana katika kutuma na kusoma meseji. Uzuri wa App hii ni kwamba ni rafiki kwa watu kwani ni rahisi sana kuitumia. Kwa hili watu wanaipenda lakini vipi kama ukiwa unataka kupata meseji zako zilizofutika?
Usiwe na wasiwasi Teknokona iko nawe. Kama ikikutokea kuwa unahitaji kupata meseji zako ulizozifuta kwa bahati mbaya hata kwa makusudi kuna njia mbadala ambayo unaweza ukaitumia katika kupata meseji hizo.
Jinsi Ya Kufufua Meseji Zilizofutika Katika WhatsApp.
Hapa ntakupa njia mbili ambazo zinaweza zikakusaidia. Njia hizi zitajalisha kama meseji zako zimefutika muda mrefu uliopita au hivi karibuni. Njia mbili zote hizo zina namna yake ya kufanya.
Kama Meseji Imefutika Hivi Karibuni
Ni rahisi sana kufufua meseji katika mtandao wa WhatsApp kama zimefutika ndani ya siku 7. Kila siku WahtsApp huwa wanafanya ‘back up’ ya meseji zako zote na kuzihifadhi katika memori kadi yako. Unaweza ukaitumia ‘back up’ hiyo kufufua meseji zako zilizofutika
Ili kulipata meseji zako zilizofutika katika WhatsApp kwa kutumia ‘back up’ uliyoihifadhi fanya hivi; futa WhatsApp yako na kisha ipakue tena katika simu yako. Ukishamaliza kuipakua wakati wa kufungua mtandao huo utakuomba urejeshe taarifa zako. Unaweza kurejesha mpaka meseji za siku saba tuu kwa kutumia njia hii
Kama Meseji Imefutika Zaidi Ya Siku 7 zilizopita
Hapa itakubidi utumie njia nyingine kabisa katik akuhakikisha unapata kuzifufua meseji zako. Taarifa zote ambazo hazikuhifadhiwa hazitaweza kupatikana tena kwa kutumia njia hii
Njia
1. Shusha ‘File Manager’ kutoka google Play
2. Futa WhatsApp Katika Kifaa chako
3. Kwa kutumia ‘File Manager’ nenda katika faili la /sdcard/WhatsApp
4. Utaona mafaili ambayo yanafana hivi
5. Chagua tarehe yeyoteili kufufua faili la tarehe hiyo. Baada ya hapo badilisha jina la faili hilo kwenda msgstore.db.crypt
6. Weka WhatsApp tena katika kifaa chako na kisha chagua kurudisha taarifa zako (restore). Hapo faili la msgstore.db.crypt ndio litakalojirudisha katika simu yako hivyo utapata meseji zote za siku hiyo kwa mara nyingine tena.
Mpaka hapo utakuwa unaweza kufufua meseji zilizofutika katika WhatsApp. Hii itaweza kukusaidia sana kama kuna meseji ambazo unataka kuzifuta kwa muda au hata zile ambazo umezifuta kwa bahati mbaya. Cha msingi ni kwamba kabla hujafuta WhatsApp yako hakikisha umehifadhi taarifa zako vizuri.