Simu ya iPhone 5 kutoka kampuni ya Apple imeweka rekodi ya kuwa Smartphone nyembamba zaidi kwa kipimo cha 7.6mm. Simu hii ilizinduliwa siku ya Jumatano nchini Marekani, na wengi watasema itafanya vizuri katika soko la ushindani la simu linalozidi kukua kila kukicha.
Ukilinganisha iPhone 4S Kushoto na iPhone 5 Kulia |
Pia iPhone 5 imekuja na kioo kikubwa zaidi hii ikiwa ni mabadiliko ya kwanza ya ukubwa wa kioo ‘display’ tangia Apple watoe iPhone ya kwanza hapo mwaka 2007. Baada ya kuona simu zenye vioo vikubwa za Android zikifanya vizuri sokoni kampuni ya Apple imeamua kuongeza ukubwa display katika iPhone 5 kwa kipimo cha inchi 4. ( resolution = 1,136 x 640 pixels).
Kioo: iPhone 4S Kushoto, iPhone 5 Kulia |
iPhone 5 ina uzito wa gramu 112 kulinganisha na gramu 140 za iPhone 4S, pia kwa wembamba toleo lililopita la iPhone, 4s, ilikuwa na wembamba wa 9.3mm.
Pia zimekuja na spika za masikio (earphones) mpya kiubunifu, baada ya miaka mingi bila kufanya mabadiliko ya spika kampuni ya Apple imeleta spika za masikio za ubunifu wa hali ya juu na pia zikiwa zinafanya kazi vizuri zaidi. Spika hizi zimepiwa jina la EarPods.
Pia kamera yake inauwezo wa kupiga picha haraka zaidi na katika hadhi (quality) nzuri zaidi kwa zaidi ya asilimia 40 zaidi kulinganisha na toleo la iPhone 4S. Kamera ya mbele ni ‘High Definition’-HD na ya nyuma ni 8MP.
iPhone 5 inakuja na programu mpya ya uendeshaji kutoka Apple, iOS 6 kulinganisha na 5.1.1 iliyopo katika iPhone 4S na iPad 3. Ila hapo tarehe 19 mwezi huu iOS 6 itakuwa tayari kwa watumiaji wote wa iPhone 4, 4S na iPad 2 na 3 kwa ajili ya kushusha (download & upgrade).
Mabadiliko mengine makubwa yanahusu mfumo wa kuchaji, iPhone 5 imekuja na mfumo mpya hivyo chaja za bidhaa zingine za Apple kama iPhone, iPod na iPad zilizopita hazitaingiliana na iPhone 5. Mfumo huu mpya unaitwa ‘Lightning Connector’ ni tofauti sana na charger zilizopita zilizokuwa pana zaidi.
Kuhusu bei, iPhone 5 itapatikana kwa dola za kimarekani 649 kwa uhifadhi wa GB 16, uhifadhi wa GB 32 itauzwa kwa dola 749 na mwisho kwa ile kubwa zaidi ya uhifadhi wa GB 64 itakuwa takribani dola 849.
Simu hii itaingia sokoni rasmi hapo tarehe 19 mwezi huu, na ndiyo simu pekee inayoweza ikaleta ushindani kwa Samsung Galaxy SIII kutoka kampuni ya Samsung.
No Comment! Be the first one.