fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Smartphones

Ifahamu WhatsApp Messenger

Spread the love

Kwa watumiaji wa simu za Blackberry waliojiunga na Blackberry services wanafurahia huduma ya kutuma ujumbe wa maneno, sauti, picha pamoja na video kwa kutumia application ijulikanayo kama Blackberry Messenger (BBM) huduma ambayo imejipatia umaarufu mkubwa hasa kwa vijana.

Kama nilivyodokeza mwanzo huduma ya Blackberry Messenger ni kwa ajili ya watumiaji wa simu za Blackberry tu ila kwa wale watumiaji wa simu zingine hatupaswi kunung’unika tena Kwani Kampuni ya WhatsApp Inc ya huko Silicon Valley Marekani imetoa njia mbadala kwa kutengeneza application inayotoa huduma karibu sawa na Blackberry Messenger iliyopewa jina la WhatsApp Messenger. Cha kufurahisha zaidi Application hiyo inaweza kutumika kwenye simu za Nokia, Iphone, Blackberry pamoja na simu zote zinazotumia mfumo wa Android (kwa wale watumiaji wa simu za Kichina ya kwenu labda baadae sana).

Application hii ya WhatsApp Messenger inatolewa kwenye mtandao – www.whatsapp.com – ikiwa na mwaka mzima wa kuitumia bure na Baada ya muda huo kuisha unaweza kuinunua kwa kiasi cha dola moja tu.

Ili kuwasiliana kwa kutumia Application hii Inabidi wewe pamoja na yule unaehitaji kuwasiliana nae muwe mmefanya installation ya WhatsApp Messenger kwenye simu zenu.

SOMA PIA  Kuwa Tayari Kwa Emoji Mpya Na Nzuri Zaidi!

WhatsApp messenger inafanya kazi kwa kutumia huduma ya internet kwenye simu yako hivyo hauitaji kulipia gharama za ziada kutumia huduma zote zinazotolewa na application hii hivyo ni njia nafuu zaidi unayoweza kutumia kuwasiliana na rafiki zako, una Kila sababu ya kuijaribu.

Ili kufahamu na kupata mapendekezo ya Applications zinazostahili kuwa kwenye simu yako endelea kutembelea blog hii.

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Comments

  1. Abdallah Aflah Mohammed - September 26, 2014 at 15:55 - Reply

    nina ipad ina ios8 inaingia whatsapp

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania