Juzi juzi tuu nimetoka kugusia kuhusiana na mauzo ya vifaa vya Playstation Kutoka Sony, leo ni zamu ya GTA 5 huku ikiwa imetimiza mauzo ya mamilioni.
Ni wazi kuwa soko la magemu linakua kwa kasi sana siku hizi, na wawekezaji wengi wanaangalia sekta hiyo kwa jicho la tatu. Leo tugusie katika swala hili la GTA 5

Kampuni ambayo inahusika na uchambuzi na uchapishaji wa magemu, Take-Two imesema kuwa gemu la GTA limeweza kuweka rekodi hiyo ya mauzo ya nakala milioni 170 kwa gemu ya GTA 5 pekee, huku kukiwa na mauzo ya milioni 70 kwa gemu lingine lijulikanalo kama Red Dead Redemption.
Katika repoti ambayo kampuni imeitoa ni kwamba magemu ya GTA (ule mwendelezo) yameuzika kwa zaidi ya nakala milioni 385 huku GTA 5 pekee ikiwa ni nakala 170 na zaidi.
GTA ni moja kati ya magemu ambayo yameuza sana na tena kwa haraka ukifananiasha na mauzo ya magemu mengine.
Hapo ni kuongelea nakala tuu, lakini ni wazi kuwa magemu mengi yanayomilikiwa na kampuni ya Rockstar huwa yanapata mauzo ya juu kabisa.
GTA 5 pekee ndio kiburudisho (kifaa cha burudani) pekee ambacho kimeuza haraka mpaka kufikia mauzo ya dola bilioni moja –hii haijawahi kutokea wala kuvunjwa na namba hiyo ilipatikana ndani ya siku tatu tuu.
Pengine muendelezo wa magame ya GTA huwa yanakua yakisubiriwa kwa hamu na watumiaji duniani kote, lakini vile vile magemu haya huwa ni mazuri sio?
Chanzo: IGN
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani gemu hili litaendelea kuuza nakala nyingi zaidi na kunedelea kuvunja rekodi kabla ya GTA 6 kutoka?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.