Mortal Kombat ni gemu la kupigana lenye zaidi ya wachezaji 37 na linaloruhusu watu wawili kucheza kwa pamoja kupitia mtandao au bila mtandao. Unaweza kupakua au kunua gemu hili mtandaoni na kucheza kupitia kompyuta yako au runinga lako.
Gemu la Mortal Kombat lilitengenezwa na kampuni ya Midway Games mwaka 1992. Lakini kwa sasa gemu hilo linamilikiwa na kampuni ya Warner Bros. Kutokana na umaarufu wa gemu hili zilitengenezwa filamu mbili zenye hadithi iliyopo kwenye gemu hilo kuhusu wachezaji wake. Filamu hizo ni pamoja na Mortal Kombat (1995) na Mortal Kombat: Annihilation (1997).
Kuna matoleo 11 ya gemu la Mortal Kombat tangu lianzishwe. Matole ya zamani kama toleo la kwanza mpaka la nne yalikuwa ni magemu aina ya Arcade ambayo huwekwa kwenye mashine maalum ili uweze kucheza. Matoleo yaliyofuata baada ya hapo yalikuwa yanapatikana katika Playstation jambo ambalo lilipelekea gemu hii kupata umaarufu zaidi.

Unaweza ukachagua mchezaji yupi unayetaka kumtumia katika gemu hili. Kuna zaidi ya wachezaji 37 katika gemu hili ikiwemo Sonia, Johny Cage, Scorpion na Sub zero. Unapocheza gemu hili kupitia playstation unaweza kutunza kumbukumbu za ulipoishia ili unaporudi tena usianze mwanzo kucheza.
No Comment! Be the first one.