Kampuni ya Foxconn inayomiliki viwanda vikubwa vinavyotengeneza parts na ata vifaa mbalimbali kwa ajili ya Apple na Samsung yaanza kutumia roboti zaidi katika viwanda vyake na hivyo kupunguza wafanyakazi kwa kiasi kikubwa.
Inasemekana wafanyakazi 60,000 hivi karibuni walipoteza ajira zao na nafasi zao kuchukuliwa na roboti.
Mtandao wa South China Morning Post ulimkariri afisa mmoja wa serikali akisema kiwanda kimoja cha kampuni hiyo nchini China kimepunguza wafanyakazi kutoka wafanyakazi 110,000 hadi kufikia 50,000 kutokana na utumiaji wa maroboti katika kazi.
Soma Pia – Roboti atakayemezwa ili kusaidia kutoa uchafu na kutibu tumboni! #Teknolojia
Ukuaji wa teknolojia za utengenezaji roboti wenye uwezo wa kufanya kazi ndogo ndogo zinazohusisha upangaji na upachikaji wa vitu inasemekana utasababisha upotevu wa ajira kwa watu wengi sana maviwandani.
Wenyewe Foxconn wamejitetea pale walioulizwa na shirika la BBC kuhusu jambo hili wakisema wanatumia teknolojia ya roboti katika kazi ambazo ni za kawaida sana na hivyo kuwafanya wafanyakazi wa kawaida kuhusishwa tuu katika majukumu mengine ya kikazi yanayohusisha vitu kama vile utafiti na usimamiaji wa ubora wa bidhaa.
Inasemekana kuwekeza katika mkono wa roboti mmoja kwa ajili ya ufanyaji wa kazi za kama vile kuunganisha kitu kimoja gharama yake ni takribani dola 35,000 (Tsh Milioni 76.7 | Ksh Milioni 3.5).
Ukilinganisha na kama kazi inayofanywa na roboti huyo ingefanywa na mtu basi mtu huyu angelipwa si chini ya dola 15 kwa saa (Tsh 32,000/= | Ksh 1,500/=), kwa kazi ya takribani mwaka mmoja basi malipo kwa mtu yatakuwa ni zaidi ya dola 70,000.
Ukilinganisha pia ufanyaji kazi wa mwanadamu una mambo ya kuangalia kama vile uchovu, likizo, malipo ya kodi kwenye mshahara, malipo ya bima n.k unakuta ya kwamba kama kazi hiyo itafanywa na roboti gharama kwa wenye viwanda inashuka kwa zaidi ya nusu.
Wengi wanaona huu ni mwanzo tuu ila tunavyozidi kwenda mbele ndio tutazidi kuona utumiaji wa maroboti katika kazi nyingi za viwandani zinazofanywa na watu kwa sasa.
Soma Pia – LAUNDROID: Panasonic Waja na Roboti kwa Ajili ya Kufua, Kukunja na Kupanga Nguo
Tuambie, unadhani itafika muda kutakuwa na ugumu wa ajira uliosababishwa na utumiaji wa maroboti zaidi?
[socialpoll id=”2363006″]
Chanzo: BBC