Amazon ina huduma ambayo inaiita Alexa, kazi kubwa ya huduma hiyo ni kuwa kama msaaidizi wa mtu (kama vile Siri kwa Apple) ambapo kinapoamuriwa kinafanya kazi ndogo ndogo kama vile kupiga muziki n.k
Huudma hii kutoka Amazon ina uwezo wa kujibu kile kitu ambacho inaambiwa, kwa kipindi cha muda imekuwa kitoa majibu kwa kutumia sauti za watu maarufu kwa kupitia mfumo wa spika.

Watu maarufu hao ni kama Samuel L. Jackson, Shaquille O’Neal, na Melissa McCarthy ambao wote sauti zao zimetolewa katika huduma hiyo.
Kingine ni kwamba sauti hizo zilikua hazipatikani bure, ilikubidi ununue sauti hizo ile ziweze kutumika katika kifaa hicho.
Kilichotokea ni kwamba kwa sasa mtu utashindwa kuzinunua sauti hizo, na kama ulishazinunua basi utazitumia mpka pale muda utakapo fika.
Kwa sasa ni kwamba sauti ya Jackson itatumika mpaka kufikia juni 7 huku za wengine hao wawili (shaq na McCarthy) zitafika mpaka septemba 30 mwaka huu.
Sauti hizi zote wakati zinatoka ziliuzwa kwa dola 0.99 za kimarekani baada ya mapokeo kuwa makubwa zilipanda mpaka kufikia dola 4.99 za kimarekani.
Amazon haijaweka wazi juu ya kwanini inafanya hizi –kuondoa sauti hizo—lakini inaonyesha sdhari kwamba haitaki kuytengeneza hela kupitia njia hiyo au kwa watu hao.
Wengine wanasema pengine hili limetokea hili kwa sababu Amazon wenyewe wanataka waongeze huduma inayofanana na ChatGPT katika Alexa.
Kwa dunia ya sasa hili sio jambo geni kabisa, maana kwa sasa ni makampuni mengi yanatumia huduma ambazo zinapatikana kwa kutumia teknolojia ya AI.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Wewe unahisi sababu ni nini mpaka kampuni kuzitoa sauti hizo?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.