Hapo alhamisi, siku mbili zilizopita Baraza la Umoja wa Mataifa linalosimamia masuala ya Haki za Binadamu walipitisha azimio lililofanya kupata huduma za intaneti kama haki yako kama binadamu.
Azimio hilo linasema watu wote wana haki ya kupata na kutumia huduma ya intaneti, pamoja na kujielezea kwa uhuru kupitia intaneti. Nchi 47 zote zinazotengeneza baraza hilo zilipitisha azimio hilo na hii ni pamoja na mataifa mawili yanayolalamikiwa kwa kutoruhusu uhuru mkubwa wa kujieleza, nchi ya Uchina na Cuba.
Kwa upande wa Uchina walisema wamekubali azimio hili kutokana na moja ya sentensi iliyokatika azimio hilo inayosema ‘mtiririko huru wa habari kwenye mtandao na mtiririko salama wa habari kwenye mtandao ni pande tegemezi’, mjumbe kutoka Uchina, Bwana Xia Jingge aliiambia kamati hiyo kuonesha Uchina haipo tayari kubadilisha sheria zake maarufu kama Ukuta Mkubwa wa China (Great Wall of China).
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ni chombo ambacho hufuatilia maendeleo ya haki za binadamu na ukiukwaji wake katika nchi zote wanachama. Baraza hili limeeleza haki ya uhuru na kujieleza “moja ya misingi muhimu ya jamii ya kidemokrasia” na imetambua umuhimu wa intaneti katika “kuendeleza na kulinda haki ya uhuru wa maoni na kujieleza.”
No Comment! Be the first one.